Kabla ya kumvulia nguo mwanaume mme wa mtu ebu jiulize Mambo yafuatayo!

➡️Kwanini hakukuoa wewe?
Kama kweli ungekua Ni mtu wa thamani kwake na Kuna kitu anakiona kizuri kwako ambacho anajua kinamsaada mkubwa kwenye kujenga familia yake angekuoa lakini kwakua huna sifa na vigezo vya wewe kujenga familia pamoja ndio maana anaishia kukutamani tu na Kama anakwambia anakupenda fahamu kua anakudanganya. Anakutumia tu na baada ya siku hautakua nae kwa sababu Hana anachokipoteza kwako

➡️ Kama amepata ujasiri wa kukutamani wewe fahamu kua Kuna wengine wengi amewatamani na wewe siyo wa Kwanza, usidhani kua utakua wewe peke yako kwa sababu tayari Ni tabia ambayo anayo na kila atakapomwona mwingine atamtamani na kuanza mahusiano naye, kwahiyo uki expire atakuona wa kawaida Kama anavyowaona wengine wa kawaida akiwemo mke wake! Na hili kwa wanaume inabidi kubadilika na kulizika na mke wako, unachokitafuta nje hakipo kizuri zaidi ya mke wako, kipendezeshe Cha kwako,ukiwa na shauku ya kwenda lodge mwandae mke wako mtoke naye na ukitaka kwenda out toka naye, Mfurahie mpaka aumbike moyoni mwako!!

➡️Fikiri juu ya mwanamke mwenzako aliyeachwa Nyumbani na wewe umemng'ang'ania!

Licha ya kua na watoto pia kumbuka kuna mwanamke mwenzako anateseka na watoto huku uchumi wote umeushikilia,kuna watoto wanataka ada ya shule, mwanamke mwenzako anaumia Sana na anatokwa na machozi kwa ajili yako. Fikiri ungekua wewe ungejisikiaje? Kwanini unamdondoshea machozi mwanamke mwenzako?
Unamganda mpaka amesahau Nyumbani,hawezi Tena kuacha matumizi Wala kuwaona watoto wake. Watoto wanaumia sana kutokumwona baba yao Nyumbani mapema! Inauma Sana Sana, naomba umwachie huyo mwanaume akatunze familia yake na kufurahia na watoto wake! Kwa kufanya hivyo Mungu atakuvusha hapo ulipo na atakupa mme wako bora, huyo siyo wa kwako!!

Marriage Mentorship

Ukiona kama maisha yangu yana kuuma yang' oe meno yawe kibogoyo kama bibi ako!!😂😂😂🤣
share vibwengu waone hii msg pambe

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA