MBINU TATU AMBAZO WANAUME HUTUMIA KUKUACHA KISTAARABU!

Sidhani kama ni usataarbu lakini wanaume wengi huona kama ni njia rahisi ya kumuacha mwanamke ambaye wamekaa naye muda mrefu, mwanamke hajafanya kosa lolote na walishaahidi ndoa sasa wameshindwa kumuacha kwani mwanamke ni king’ang’anizi anavumilia kila kitu. Wanaume siku hizi wanatumia mbinu hizi tatu, kuna nyingine nyingi ila leo tuangalie gia hizi tatu;

(1) Anakuomba Mapenzi kinyume na maumbile; Hii ni kubwa sana na ni kama kamtindo kwa wanaume wengi. Anataka kukuacha lakini hataki uje kumlaumu kuwa kakupotezea muda, akijua kuwa kama una akili utakataa anakuambia “Kuna kitu nilikua sijakuambia, mimi napenda kufanya mapenzi kinyume na maumbile siwezi kuishi bila hiyo kitu hivyo kama unataka tuoane basi nipe na kama huwezi basi bora kuachana maana nitakusumbua, bila hiyo kitu nitachepuka” Anategemea una akili, utakataa atakuacha, ila kama wewe ni Kizibo, utakubali atakufanyia hivyo na bado atakuacha.

(2) Anakuomba umchukulie mkopo umpe pesa kubwa;Kuna wengine anataka kukuacha lakini umekua mwema sana kwake, tena hawa ni wale ambao wanaona kuwa mwanamke ana kazi na anampenda sana anahudumia. Mwanzo ulikua unampa vihela vidogo vidogo, sasa hivi atakuomba kubwa, atakupa malengo yake mengi na mipango tenu, kasha atakuambia nichukulie mkopo kazini labda milioni 10 au 5. Anajua kuwa kama una akili utakataa, lakini kama wewe ni sijui nitumie neno gani hapa, ila utakubali ukikubali atazichukua na kukuacha atakuacha.

(3) Anakuambia kuwa kwao hawataki kabila/wamekukataa; Akishafanya mambo yote yakashindikana, umekua king’ang’anizi hutaki kumuacha basi hii ni karata ya mwisho. Siku zote alijua wewe ni mchaga lakini baada ya miaka mitatu ndiyo anakuambia kuwa kwetu hawataki wachaga (ni watani zangu) siku zote alijua kuwa wewe ni dini tofauti leo anakuambia hawataki hata ukikubali  kubadili au mwingine anakuambia kuwa kuna mwanamke nimetafutiwa, ndugu yangu hapo ondoka tu, acha kujilazimishia na kujiulizia maswali mengi, ni kwamba ushaachwa basi maisha lazima yaendelee acha kuomboleza sana.

Nishamaliza usisahau tu kusoma kitabu changu cha #NdoaYanguFurahaYangu

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA