KAMA KAKUTONGOZA KWENYE MITANDAO NA HUJAONANA NAYE BADO MHESABIE KAMA TAPELI!





Nimekaa sehemu mtaani, niko na rafiki zangu wawili, ni wadada, wapo na rafikiyao mmoja ambaye simfahamu, akapigiwa simu, akanyanyuka na kenda kuongea, basi akaongea kama nusu saa. Baada ya muda akarudi, ana Blash, si unajua ten aile kizungu, hata hakujali kuwa niko pale, mara ukasikia.
“Kelvin anakuja, sijui nitamuambia nini mume wangu maana, nataka ni spend the whole day na yeye…” wakaanza kubishana wenzake wanamuambia.
“Mwanaume mwenyewe humjui, hujawahi kumuona, unataka ukalale naye4, kwanini msisalimiane kwanza mkajuana ndiyo u spend naye!” Dada hajakubali, nimeka kama lifala flani pale, si unajua uko na wadada halafu wanaongea mambo yao kama vile husikii, yaani wanakuona kama mwanamke mwenzeo.
Unawacheki tu, nikataka ninyanyuke lakini kuna kitu kikaniambia hapana, kwanza unapewapewa kajoto uondoke uende wapi? basi wakabishana wewe, dada anataka kumuona huyo Kelvin wake wake waliokutana mitandaoni.
“Mnaona alivyo Hansome, aisee, angalia, hapana naonana naye!” Anaongea huku akipirisha simu kuwaonyesha wenzake, ikapita na kwangu ili kumsogezea mwingine maana niliwekwa katikati (nina kichaa nani akae pembeni) basi kuona picha tu na ile profile nikajua kuwa huu binti kapigwa. Nikawaacha wakaongea ongea kama wamechanganyikiwa mwisho nikawaambia.
“Huna haja ya kumuoga mume wako, huyo mwanaume haji?” Wote kama wamashtuka kutoka usingizini, wakaniangalia kama wanataka kunisuta.
“Huyo Kelvin wako ni Feki, hizo picha anazoweka si za mtandania, huo uhandsome si wa mtanzania…” wakaanza kunishanga, akabwabwaja na kusifia, anavyoweka status, anavyoongea na kuongea mengi. Mpaka nikatamani kumuambia unaongea na Iddi Makengo na kakuambia kuwa huyo mtu ni fake kubali, ila nikatulia, nikachukua simu yake, nikaanza kuangalia picha za huyo mtu.
Aisee dada zangu mnadanganywa kifala sana, kwanza angalia magari anayoweka, usukani uko kushoto, mnajua kuwa hayo magari ni ya marekani nan chi nyingi za ulaya kibongo bongo mengi yapo kulia. Lakini achana na hiyo, hizo barabara, yaani kuna lami la kibongo na lami la huko ni vitu viwili tofauti kabisa, achana na hiyo, nyumba tu za kule, hata kama si maghorofa lakini kuna namna ambazo zipo mpaka mtu unajua hapa si bongo.
Nikamuonyesha vitu vingi sana mpaka akachanganyikiwa, unajua yule mtu aliyekua xcited, yaani alishafika kileleni halafu umuambie kuwa umeitwa kazini ndiyo hiyo dada, yaani akawa kama mashabiki wa Liverpool wamebakiza mechi mbili ubingwa wanaambiwa Corona. Nilimuambia huyo mtu ni tapeli. Lakini nikamuambia tongoza ya jamaa ni lazima ipo straight, yaani anajiamini, anajua anachotaka, yaani mwanamke unatongozwa mpaka unajiozesha, mwanaume hazunguki zunguki yuko moja kwa moja.
Akaniuliza umejuaje, nikamuambia nimejua tu, basi akawa haamini amini, nikamuambia Dada naweka milioni mbili wake laki moja kesho akija unachukua. Hakuweka ila nikamuambia, kesho mtaonge vizuri, amekuambia anakuja na basi au gari, akasema gari, private, nikamuambia basi kesho utapigiwa simu na mtu humjui atakuambia Kelvin wako amepata ajali wanahitaji pesa kiasi flani akikuambia hivyo utanipigia kunishukuru, ukituma umeliwa.
Sikumpa hata namba yangu ial kesho yake alinitafuta na kuniambia jamaa yake kapata ajali wanaomba laki tano. Nikamuambia waambie wasubviri afe wakachukue maiti. Basi hakuamini nilijuaje ila nilimuambia, ingia inbox futa meseji zote za huyo mtu na mblock, kwakua hukutuma picha za uchi hawezi kukufanya chochote maisha yaendelee usiwasiliane naye. najua hao rafiki zako washakuambia mimi ni nani, na unanifollow sasa hivi na najua umekaa tu kimya ili nisijue ila ndiyo mimi na nimeandika baada ya kujua umejua ili na wengine wajifunze.
Kueni makini dada zangu na hawa wanaume unakuta mtu ni hansome ajabu halafu anakutongoza straight eti hana mtu au anakuambia nina mtu nataka sex tu, yaani anakutongoza mpaka unachnaganyikiwa. Wengi ni matapeli, kuna ambao wanatumia picha za watu na ambao ni wao lakini wengi ni waume za watu, sasa kama uamuacha mtu wako kwaajili ya huyo au utatuma picha zako basi itakula kwako maana wengi ni full matapeli. Kama hujawahi kuonana na mwanaume wa kwenye miandao, ukajua anafanya kazi wapi na anaishi wapi basi mhesabie kama tapeli mpaka umuone!
***NISHAMALIZA!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA