Hakuna mwanaume ambaye atakuvumilia uwe rafiki na X wako labda umtengeneze mwenyewe

 Hili swali leo nimeulizwa mara tano na nimeona niandike nirudie tena. X wako, mwanaume ambaye alishakuwa mpenzi wako akikuambia tuwe marafiki tu jua anakutaka kimapenzi hata kama alishaoa na wake mia mbili. Najua mtasema mbona wanaume wanawasiliana na ma X wao ila acha mashindano.

Hivyo kama umeolewa unajiheshimu muambie sihitaji huo urafiki, kuna sababu sio mume wako hivyo acha kumchekea chekea. Nina kesi kama tano hivi wadada wameachwa na waume zao kisa kuendelea kujichekesha chekesha kwa ma X wao. Umesahau nini, halafu kibaya ni kuwa hata kama yeye ameoa mkewe akifuma meseji zako kwake atakupigia akutukanee, mumewe atamuwakia na mke ndiyo ataomba msamaha.

Lakini wewe dada yangu, mume akikuta meseji hata kama alikuwa anakujulia hali basi atakuacha, hata mimi nikikuta eti unajichekesha kwa X nakutimua, ndiyo narudia nakutimua. Huwezi kumuacha mtu mwenye ufunguo wa kitasa cha mlango wako kwako acheze cheze hapo mlangoni wakati umeweka pesa ndani, utakuwa ni ujinga ambao ni mwanaume mpumbavu tu ataufanya.

Kama mna mtoto sawa mtawasiliana akitaka kujua mtoto anaendeleaje, lakini sio kuchat, ndiyo Baba wa mtoto wako kama wewe ni mke wa mtu hamtakiwi kuchat hata kama hujaolewa basi hakuna mambo ya kuhangaika naye, ongea naye kuhusu mtoto basi. Apige simu aulizie mtoto wake basi.

Mambo ya umeamkaje inahusu nini! Unasema ni rafiki tu unafikiri mnataka kwenda kushona sare za harusi. Kama alishakuwa X wako hawezi kuwa rafiki yako, sio kwamba muwe maadui au mkikutana msisalimiane hapana lakini acha kujichekesha chekesha na kutumiana vi emoji vya upuuzi puuzi.

Subiri uachwe ndiyo utajua kama ni rafiki yako au la, yaani kuachwa kakusababishia yeye lakini utasikia “Mke wangu hataki tuendelee kuwasiliana” Hapo upo kwenu umeshachakaa na stress za kuachwa na maisha yashakugonga. Iko hivi hakuna mwanaume ambaye atakuvumilia uwe rafiki na X wako labda umtengeneze mwenyewe.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA