Mpenzi wako anaishi mbali, Je unapaswa kuongea naye mara ngapi kwa siku?

 Hakuna kiwango maalum cha kumpigia simu mpenzi wako anapokua mbali ila angalau kuwa na kitu cha muhimu na kuwa muelewa anapokuambia yuko bize. Ingawa mawasiliano ndiyo msingi mkuu wa mahusiano ya mbali lakini yakizidi sana huwa kero hasa kama mwenza wako ni mtu wa kulalamika lalamika.

Kumpigia pigia simu mume wako, mke wako au mpenzi wako aliye mbali, ukiwa huna kitu cha maana cha kuongea, tena kwa kulalamika au kutaka akusikilize wewe tu haiwi tena mapenzi inageuka na kuwa kero.

Hapa kuna mambo mawili, kwanza ni lazima uoneshe kuwa unajiamini, hapa simaanishi kumuamini hapana kuwa unajiamini vya kutosha na kila wakati humuwazi yeye, una kitu kingine cha maana cha kufanya ziadi ya kumuwaza yeye, lakini pili ni lazima umpe pumzi na kumruhusu akumiss.

Ongea naye asubuhi ukitaka kujua hali yake, jioni kuulizia siku yake na usiku kumtakia usiku mwema na kunyegeshana. Epuka sana kuongea mchana hasa kama yeye anafanya kazi kwani si wakati mzuri, utamkuta na stress na anaweza kukujibu vibaya na kuwa mwanzo wa kuvurugika kwa penzi lenu.

Umemtumia meseji hata hajajibu basi ushampigia, umetoka kumpigia umemtumia na mesji, yuko kaitwa na Bosi umepiga, hajapokea akikupigia unaulizia mbona hukupokea, mbona hujajibu, unapiga simu mara kumi kwa siku, wewe ni kero, narudia wewe ni kero.

Ndugu yangu huo si huduma kwa wateja, atakuchoka mapema, watu wanasema sukari pamoja na utamu wake kuilamba kila saa ni kero inageuka kuwa sumu. Kama una tabia hii kupiga simu mara kumi kwa siku, halafu hakuna hata cha maana unachoongea basi jua unamkera mwenza wako.

Kama una tabia kupiga simu mchana muda wa kazi kwakuwa wewe uko ‘bored’ huna kitu cha kufanya au ushamaliza kazi zako uko free unampigia wakati yeye ndiyo kwanza bosi kamsimamia au wateja wanamsumbua jua unakera na anashindwa tu kukuambia ukweli.

Kama unataka mpigie simu muda ambao unajua kabisa katulia, hana mawazo kichwa kiko safi hapo mtaelewana. Lakini kila saa wewe tu kana kwamba wewe ndiyo Oxygen yake asiposikia sauti yako anakufa, badilika. Kulalamika lalamika kila mara ndiyo kunakomfanya asirtamani kuongea na wewe.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA