MWANAUME AKISHAKUACHA KUBALI KUACHIKA HAPASWI KUWA RAFIKI YAKO!


Najua mpo wengi, najua mnaumia, najua mnachanganyikiwa, lakini kama mwanaume akikuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine hapaswi hata kuwa rafiki yako. Narudia, kama ulikua kwenye mahusiano na mwanaume, si mahusiano yale ya tia maji tia maji, hapana!

Mahusiano yale mnapendana mpaka kila mtu anajua kuwa yeye ndiyo mume wako, lakini ghafla bila sababu akakuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine. Bado unampenda lakini kakuacha, hujamkosea kitu lakini kakuacha, alikua anakuaminisha kuwa wewe ndiyo mke lakini kakuacha.

Basi dada yangu huyo mwanaume kata mawasiliano naye, narudia, kata mawasiliano naye. Hapaswi kuwa rafiki yako achilia mbali kuendelea kuwa mpenzi wako. Najua unampenda sana lakini mwanaume kama huyo atakurudisha nyuma na utaishia maumivu tu.

Kwanza hawezi kumuacha mke wake kwaajili yako, pili hata akimuacha mke wake hatakuoa wewe kwani hakukuhitaji tangu mwanzo, tatu anakuharibia kwa wanaume wengine. Kila mwanaume akija na kutaka kukuoa anawmabiwa una mtu wako kumbe ni mume wa mtu.

Narudia dada yangu achana na huyo mtu kabisa, narudia achana na huyo mtu kwani hamuachi mke wake. Anakudanganya kamuoa bahati mbaya lakini nina uhakika hakuna ndoa ya bahati mbaya, anakupotezea muda, sijui nirudie mara ngapi, najua ningumu, nitafute nikusaidie kumuacha ila usiruhusu aendelee kukutumia.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA