ACHA KUWA MWANAMKE WA KULALAMIKA TU, TAMBUA JUHUDI ZA MUME WAKO


Moja ya sababu kubwa za wanaume wengi kuchelewa kuoa ni kujiandaa kiuchumi kwaajili ya kutengeneza familia.  Mwanaume amelelewa na kukuzwa katika jamii ambayo inaamini kua katika familia ni jukumu lake kuhudumia famila yake kiuchumi na kuhakikihsa mke na watoto wake wanakuwa na maisha mazuri.

Hii ndiyo maana kijana hukakikisha kuwa anakua na uwezo wa kuhudumia familia kabla ya kuoa. Tofauti na mwanamke ambaye anaweza kuolewa hata bila kuwa na kazi na akaendelea kubaki kuwa Mama wa nyumbani katika maisha yake yote ya ndoa, mwanaume hawezi kufanya hivyo.

Hata kama mkewe atakuwa na kila kitu, kwa maana ya pesa lakini bado mwanaume atahitaji kufanya kazi na kuchangia chochote ndani ya familia. Huo ndiyo uanaume, mwanaume kamili hujisikia vibaya pale anapokuwa ni mtu wakulishwa na mkewe au hata tu mkewe anapokosa mahitaji muhimu ambayo alipaswa kumpa.

“Mwanamke unapolalamikia kitenge kipya, mchango wa haursi, Kitchen Party, saluni na vitu vingine hata kama si vya muhimu. Hata kama mwanaume anaona havina kipaumbele na ukivipata havikusaidii chochote, kama mwanaume hana uwezo wa kukupa basi hujisikia vibaya kwani ataanza kujiona kama si mwanaume kamili”

Hili ni suala la kisaikolojia kwamba anajisikia kuwa hawezi kukutimizia mahitaji yako na hata wakati mwingine huanza kuwa na wasiwasi kuwa kama yeye kashindwa kukutimizia basi unaweza kwenda kwa mwanaume mwingine kutimiziwa. Hii ndiyo sababu unakuta baadhi ya wanaume huhisi tu kuwa wake zao wanachepuka bila sababu.

“Iko hivi hata kama umemuomba kitu ambacho angekuwa na hela asingekupa lakini kwakua kashindwa kukupa kwasababu hana pesa basi jua kuwa atajisikia vibaya kwa kushindwa kukuhudumia kama mke wake”.

Kwasababu hiyo basi kama mwanamke unapaswa kua na akili na kuomba kutokana na uwezo wa mume wako, mke bora ni yule ambaye anatambua uwezo wa kifedha wa mume wake na kujizuia kuomba vitu ambavyo si vya muhimu na ambavyo ana uhakika kuwa mumewe hana uwezo navyo.

Unapoomba kitu ambacho mumeo hana uwezo nacho ni kutengeneza migogoro ambayo haina msingi. Kwanza utamfanya mume wako kujisikia vibaya kwa kujiona kuwa si mwanaume kamili kuweza kukuhudumia, lakini pili unaanza kumpa mashaka ya kuanza kukufuatilia. Hata kama utajikusanya na kununua kile kitu akili yake itaenda kwa mwanaume mwingine kama ukiweza kununua mwenyewe.

“Ataanza kuwaza, kama mimi mwanaume nimeshindwa kumnunulia yeye kapata wapi pesa? Lazima kutakuwa na mwanaume mwenzangu anahudumia…”
Kuwa makini vitu vidogo vidogo visije kuleta mashaka katika ndoa yako. Omba vitu vya muhimu na ambavyo una uhakika kuwa vinawezekana kwa mumeo. Kama unajua anakunyima kwakua ni mbahili basi una haki ya kuomba na hata kulalamika na kununa lakini si kununa wakati unajua kuwa hana yhela ya kukupa.

Kazi ya mke ni kumsaidia mume wake, kuvumilia na kubwa kabisa kumshukuru kwa kile anachokifanya. Onyeshakuwa unajali na unamshukuru kwa juhudi zake za kulea familia. Kwamba anavyohangaika kila siku unakubali na unatambua kua anafanya kila kitu ili kuhakikisha familia yake inakula na kuishi vizuri.

Mshukuru na muambie kuwa yeye ni bora, acha kuwa mtu wa kulalamika. Hakuna kitu ambacho kinakera wanaume wengi kama kelele za malalamiko kuwa hawawezi kutimiza majukumu yao ya uanaume. Kwamba ametoka kazini amehangaika sana, ametukanwa na bosi na kudharauliwa na wafanyakazi wenzake, akapata alichopata halafu anaenda kwa mkewe nayeya namdharau na kununa kila saa.

Acha kumkatisha tamaa mume wako, mke unapaswa kuwa mtu wa kwanza wa kumpa moyo. Kuwa kimbilio lake pale anapokuwa na stress, acha kumsukuma mume wako na kumfanya kuiona nyumba yake kama kazini kwake, mpe amani na muambie kuwa anajitahidi na bado ana nguvu ya kufanya zaidi. Usipo mpa moyo na kufurahia kidogo anachofanya basi jua kuwa atatafuta mtu wa kumfanyia hivyo.

“Kila mwanaume anataka amani katika nyumba yake, kama hutampa amani basi atatafuta mtu wa kumpa. Amani ya roho ni kama maji ya mto ukiziba upande mmoja wa mto yatatafuta upande wapili wa kupita na maji yakikosa pakupita basi yataondoka na wewe.”

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA