UKIWASIKILIZA WATU HAWA SANA UNAWEZA KUCHANGANYIKIWA KUHUSU NDOA!


Moja ya sababu kubwa ya wanawake kuteseka kwakua tu hawajaingia kwenye ndoa ni ndugu. Kuna presha kubwa ya ndugu, majirani na sehmeu za ibada kwa mwanamke hasa anapofikisha miaka 30 bila ndoa. Wengi huona kama ndiyo maisha yake yameisha kwamba anahitaji kuwa na mwanaume ndiyo awe na furaha.

Ndugu humtenga, marafiki humtenga na hata katika nyumba za ibada kuna vitu vingi hatakiwi kushiriki kwakua tu hajaolewa. Hii huwapelekea wanawake wengi kuingia kwenye ndoa za mateso bila kufikiria mara mbili ili tu kuridhisha jamii na wao kuonekana wameolewa.

Kama uko katika hali hii unapaswa kujua mambo makuu mawili. Jambo la kwanza nikuwa, ndoa hupangwa na Mungu hata hao wanaokupigia kelele kuwa utaolewa lini hawakujipangia ndoa na siku zote wakati wa Mungu ndiyo wakati sahihi. Hivyo hivyo kwa mtoto, hupangwa na Mungu na wala mtoto haletwi na ndoa au kelele za ndugu zako.

Jambo la pili ni hivi, ukiachana na wazazi wako ambao tangu siku ya kwanza ya maishaa yako wao hukutakia mema wengine wote wanaokuuliza kuhusu kuolewa kwako ni wanafiki na hakuna wanachojali kuhusu wewe. Ukiangalia wengi wao wapo kwenye ndoa ambazo ni za tiamajitiamaji na ni kama wanakuonea wivu kuwa unafuiraha bila ndoa na wao wana ndoa bila furaha.

Usiingie kwenye ndoa kwakua tu unadhani umri umeenda, usiingie kwenye ndoa ili kuwafurahisha watu bali tafuta mtu ambaye unahisi mtaendana naye. kitu cha pili acha kujihukumu, acha kusikiliza maneno ya watu kwani yatakufanya kujidharau na kujisahau hivyo kuwa mtu wa huzuni na wanaume kukukimbia.

NB; AMINA; NI post inayofuata, soma utanielewa zaidi.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA