MWANAUME WA MITANDAONI AKISHAANZA HIVI JUA NI MUONGO!


Umeshawahi kukutana na mwanaume kwenye mitandao ya kijamii, mkawa mnachat mkazoeana, akakupa stori moja namna alivyoachana na Girlfriend wake, lakini labda akakuambia kuwa yeye ana mtu lakini hawako siriasi, akakueleze vikasoro vikasoro vya huyo mtu. Ukiangalia zile kasoro unaona ni za kweli kwamba hata wewe zinakukera na kiukweli ana haki kutokuvumilia.
Kuhusu kuachana na X wake, atakuambia labda alimfuamania na rafiki yake, au akakuambia kuwa walikua wanapendana sana lakini suala la dini likawa tatizo au ndugu zake tu hawakumpenda. Lakini utamsikia kuwa alikua anampenda lakini binti alikua hajawa tayari kuwa kwenye mahusiano siriasi, utamsikia akisema mimi nilitaka twenda next step lakini akaseama yeye bado.
Yaani atakupa victory ambavyo vitakufanya uwaze “Wanawake wengine ni wajinga yaani unamkataa mwanaume kwasababu hii na hii!” Sijui unanielewa, unakuta vile vitu ambavyo wewe unavitamani kwa Boyfriend wako, ndiyo anavyo na ndiyo mwanamke mwenzako anakataa. Labda anakuambia mapenzi yalikua ya mbali lakini hapendi kuchat, si mtu wa kupokea simu, utasikia alikua karibu sana na marafiki zake kuliko mimi na vitu vingine kama hivyo.
Sasa kabla sijakuambia kitu kingine kuwa kama unakutana naye wa namna hiyo jua ni muongo! Narudia ni muongo, lakini huo uongo si mbaya ni mbinu tu ya kutongoza hivyo usimuache, jua ni muongo lakini uongo mtamu kidogo maana na wewe unaupenda. Sasa ngoma inaanza katika kuchat, akishaanza habari za umevaa nini, sijui ukoje huko, anataka video chat na anataka kuona mwili wako wakati mnachat.
Haishii hapo, ataanza nitumie vipicha, mwanzo vya kawaida, ila baada ya muda ni night dress na mwisho anakuomba picha za uchi. Sasa haishii hapo, ukikataa kumtumia hizo picha anakasirika kabisa, unaona kanuna, anaweza kuacha kuchat, kukata simu na hata kujifanya kununa.yaani ananuna na kupunguza mawasiliano kwakua umekataa kumtumia picha za ajabu ajabu. Anaanza kukuambia kuwa inamaana huniamini au hauko siriasi na mimi.
Haishii hapo ananuna na kukuambia sasa kama mwanzoni hivi hatuaminiani huko mbeleni itakuaje. Hawa watu wanashawishi aisee, anakuambia antaka kuona viungo vyako, anataka kila wakati awe anawaza mwili wako kwani hataki kurukaruka. Sasa najua ataongea vitu vingi na wewe kama ni mgeni wa haya mambo, sikuiti mjinga hapana ni mgeni labda ukasema kwani bei gani?
Ukaamua umtumie, lakini ukatuma vipande vipande ukaamua kukata uso, hapo anakasirika, anakuambia hivyo ha enjoy, anataka kukufurahia wewe, kukuona, anakuambia sasa hivyo vipande ningetaka si ninge Google tu! Najua bado unachat naye, labda wewe ni mjanja umekataa ujinga wake, unamuambia picha hutumi, anakasirika anakata mawasiliano, ukimtafuta anajifanya yuko bize na sababu nyingine nyingi.
Wengine hata wanakuambia,chagua kama unataka tuwe wapenzi siriasi au marafiki wakawaida, kwani mimi siwezi kuwa na mpenzi ambaye hata siujui mwili wake. Dada mpaka hapo huyo mwanaume ni shetani na kama unataka kuumia basi endelea naye, narudia muache. Kuna sababu tatu, kwanza nikuwa amekudanfanya haajachana na Girlfriend wake, anaye na pengine yuko hapo pembeni wakati anachat.
Lakini inawezekana ana mke kabisa, na mkewe ni hawa ambao wanalazimika kununua Kitabu changu ili kunusuru ndoa zao kwakua wanaume wako bize na laptop kuomba picha za watu. Lakini tatu nikua wewe si spesho, huyo mwanaume nikuwa hachat na wewe tu, hapana, katika mitandao aislimia kubwa ya wanaume huchat na wanawake zaidi ya kumi kwa wakati mmoja, kwamba hata meseji nyingine ni copy na paste.
Hata wakati anaanza alindika meseji moja na kuituma kwa wanawake zaidi ya kumi na waliojibu ndiyo aliendelea nao. Sasa hata katika picha za uchi atawaomba wote na watakaotuma ndiyo ataendelea kuwachora kila siku. Watakao kataa basi atawapotezea kwani yeye lengo hata halikua kukuona bali kukudhalilisha kwa kuangalia picha zako za uchi sasa kama hutumi ahangaike na wewe ya nini?
Ndiyo maana ukikataa tu unakuta anajifanya kukasirika na kukatisha mazungumzo. Hivyo dada yangu kama una mwanaume, hata humjui na kashaanza kukuomba picha za uchi wewe chakufanya mblock tu. Sisemi katika mitandao watu hawapendani, hapana wapo na wengine huoana, lakini kama hakuhesimu anaomba ujinga jua kuwa huyo ni fala flani hana kazi ya kufanya anaamia kuchezea hisia za watu.
Mimi nishamaliza kwa sasa ila kama ukijisikia soma Kitabu changu, jifunze kujiamini na pia pata nafasi ya kuongea na mimi na kunielezea tatizo lako. Unaweza kuchat na mwanaume vyovyote uwezavyo lakini kamwe usitume picha za uchi, hata picha zako za kawaida unamtumia za nini, yeye ni nani au zinamsaidia nini, si aende kwenye profile yako aangalie kama wengine, hiyo ni mada nyingine ila kwa sasa ndiyo hivyo akitaka picha jua wewe ni mmoja wapo tu wa watu wake wa maonyesho!
May be an image of child and indoor

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA