NILIZAA NA SHEMEJI YANGU NATAMANI KUMUUA MWANANGU!


Natamani hata kumuua mwanangu Kaka, sijui nifanye nini, mimi bado mdogo. Mimi ni Mama wa miaka 33n nina mtoto mmoja. Wakati niko chuo nilikua nikiishi kwa dada, yangu, yeye alikua hapatani kabisa na mume wake, kila siku ilikua ni kugombana, Dada yangu alikua mkali sana hivyo kila kitu alikua akilalamika.

Alikua akimuendesha mume wake sana kiasi kwamba shemeji yangu alikua anakuja kunilalamikia mambo mengi ya dada. Kwakua nilikua naona na namjua dada yangu kwa ukali wake nilijikuta nakua karibu sana na shemeji mpaka kufikia kubeba ujauzito wake. Nilitaka kuutoa lakini shemu aliniambia kuwa ananipenda na hawezi kuniacha, alikua anatafuta sababu ya kumuacha Dada hivyo nikizaa basi inakua sababu.

Kwakua alikua ananionyesha upendo nilikubali, niliondoka kwa Dada na shemeji alinipangishia nyumba nzima nikawa naishi huko. Nyumbani walijua lakini sikujali, kila mtu alikua anamchukia dada kwani alionekana kama ana roho mbaya, hata Mama yetu alikua upande wangu, basi nilikaa hapo kwa mwaka mmoja mpaka nikajifungua.

Lakini nilipojifungua ndipo nilijua tabia halisi za shemeji, alikua ni mtu wa wanawake, hahudumii chochote. Kumbe hata kwa dada alikua hahudumii. Mimi nilikua bado niko chuo, dada ndiyo alikua ananisomesha, mwanzo nilijua pesa ni za shemeji labda dada yangu anapewa lakini haikua hivyo.

Shemu anafanya kazi lakini hatoi chochote, pes alaizokua ananipa ni za starehe tu, aliniambia atamuacha dad alakini hakumuacha, kila siku nilikua naona meseji anamuomba dada msamaha kwa madai kuwa mimi nilikua nimemuwekea dawa. Iliniuma sana lakini sikua na namna, nilikua sina kazi, nipo chuo mwaka wa pili na sikua na hata mtu wa kunilipia ada.

Maisha yalikua magumu, nyumbani napo baada ya kuona kuwa pesa hakuna, shemeji hatumi chochote walinigeuka, wakawa upande wa dada hivyo nikabaki mwenyewe. Mama yangu aliniambia nimemletea laana sitaolewa mimi na waodogo zangu hivyo nisirudi nyumbani, kodi iliisha nikawa naishi kwa rafiki yangu ila maisha yalinishinda nikajikuta naacha mpaka chuo kwani sikua na ada. Dada yangu alipoona naacha chuo hakukubali, alinilipia ada lakini akaniambia hataki kuniona, alinihudumia mpaka nikamaliza chuo, ila hakutaka niishi naye tena.

Baad aya hapo alinipa mtaji wa milioni moja na kuniambia tusijuane kwani ajira zilikua ngumu, nilianza kuuza nguo za kuzungusha na kuuza kwenye mitandao, kwa bahari nzuri nilifanikiwa kupata kazi, sasa hivi nina kazi nzuri na nina kipato kikubwa. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, dada yangu alishanisamehe kwani mume wake alishaachana naye kwasababu alikua anampiga basi akaamua kumuacha.

Lakini shida inakuja kwangu, nina mtoto, hiyo si shida, napata wanaume tena wazuri tu na wanamkubali mwanangtu, lakinis hida ni pale wakishajua kuwa mtoto nimezaa na mume wadada yangu hatwaki tena. Nimeshaachwa na wanaume watatu wote kwakua tu wamejua kuwa mwanangu nilizaa na shemeji yangu.

Hakuna hata mmoja nilishawahi kumuambia, lakini nikishamtambulisha mwanaume, akichunguza kidogo anaambiwa kuwa familia yangu si familia ya kuoa kwani tuna tabia mbaya. Kaka hali hiyo inawaathiri mpaka waodogo zangu, yaani nyumbani kila mtu ananichukia kwani nina mdogo wangu aliachwa na mwanaume wake kwaajili yangu, kwamba akioe kwetu ni kama kaoa mikosi kwakua niliza ana shemeji yangu.

Kakasas ahivi niko kwenye mahusiano na Kaka mmoja, ana miaka 40 na amefiwa na mke wake. Niko naye kwenye mahusiano ni mwaka wa pili sasa, bado sijampeleka kwetu, anataka sana kunioa kwani wanae wananipenda na anampenda sana mwanangu. Ninafanya kazi ila yeye ndiyo ananisaidia kulipa ada ya wanangu, nimemuambia Baba wa mtoto hatuko vizuri na hahudumii, yeye hajali ananiambia atamhudumia kama wake.

Shid ainakuja kwangu, bado naogopa kumpeleka nyumbani, naogopa kupata aibu nyingine tena. Naomba nisaidie nifanye nini Kaka ili nisimpoteze tena huyu mwanaume. Nampenda sana ila kwa namna alivyo, jinsi anavyojiheshimu yeye na familia yake akijua nimezaa na shemeji yengu sijui itakauje, Kaka namuona huyu mtoto wangu kama l;aaka, kama ananiharibia maisha yangu, najikuta nina hasira, namchukia sana mwanangu natamani hata afe ili aniweke huru kwenye maisha yangu, nisaidie Kaka nifanye nini?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA