UNAWEZA KUCHAGUA MWANAUME KUWA MKATILI KWAKO AU KUKUHESHIMU KWA KUJUA THAMANI YAKO KWANZA!

Matatizo mengi katika mahusiano hayatokani na ukatili wa wanaume bali uvumilivu wa wanawake. Si kama nataka kuwalaumu lakini kila ukiongea na mwanamke ambaye anapitia mateso flani katika mahusiano yake atakuambia kuwa mateso hayo yalianza taratibu. Sijawahi kukutana na mwanamke ambaye alitongozwa siku hiyo hiyo na kesho yake kuanza kupigwa.

Wengi stori zao huanza “Alinikataza kuongea na flani, alikua hataki nitoke na marafiki zangu, alikua akifuatilia simu yangu, alikua akipenda kunitukana na kuongea kwa dharau, alianza kutokunipa matumizi,alikua hapigi simu, alikua ananuna kila siku, alikua hataki kuhudumia familia, alikua ananitukana mara kwa mara.” Ndiyo matatizo mengi huanza hivi.

Katika hatua za awali wanawake wengi huvumilia na kuona kama ni kitu cha kawaida. Kuna misemo miwili ambayo wanawake wengi huitumia na kama ushaanza kuutumia mmoja wao basi jua kuwa kuna matatizo kwenye mahusiano yako. “Wanaume wote ndiyo walivyo na akinioa atabadilika” hii ni misemo ambayo wanawake wengi hutumia katika kujifariji namateso.

Wanawake wengi huvumilia, wakiamini kua wanaume wakiwaoa au baada ya kupata watoto watabadilika, lakini pia huvumilia wakiamini kua wanaume wote wako hivyo na hakuna namna ya kuwabadilisha. Wanawaza nitaachana na wangapi? Yote haya hukuza tatizo badala ya kutatua tatizo. Katika kuvumilia hivi wanasahau kitu kimoja, “Wanaume wana akili”.

Dada zangu mnasahau kuwa pamoja na kuwa mwanaume anakupiga na kukunyanyasa lakini ana akili, mambo yote anayoyafanya nikwakua unavumilia hii ndiyo maana kila unavyozidi kuvumilia ndiyo anavyozidi kuongeza dozi ya manyanyaso, binafsi sijui wewe lakini mimi sijawahi kuona mwanaume kabadilika kwakua tu mwanamke ni mvumilivu.

Hubadilika kwa sababu zake na si sababu za uvumilivu. Mwanaume akishakuona unavumilia basi huendelea kukunyanyasa lakini kama akijua kuwa mke wangu au mpenzi wangu hawezi kuvumilia ujinga wangu, kwakua ana akili basi atanagalia. Kama anakupenda basi atabadilika, hatakuletea ujinga tena, lakini kama hakupendi basi atakuacha.

Najua Dada zangu mnaogopa sana kuachwa, hasa mkikumbuka kale kamsemo mnakojiambia kuwa “Wanaume wote wako hivyo”. Lakini kiuhalisia ni bora kuachwa kuliko kuishi na mwanaume ambaye hakupendi, mateso yake ni makubwa. Ila naamini kama nakupenda basi atabadilika kama ukiamua kuwa wewe huwezi kuvumilia mateso, kama ukiitambua thamani yako mapema.

Mwanamke una nafasi mbili za kumbadilisha mwanaume anayekupenda kwa urahisi, nafasi ya kwanza ni katika mahusiano ya kawaida, na nafasi ya pili ni katika mwanzo wa ndoa yenu. Ukishachelewa kuzitumia nafasi hizi mbili inakua ngumu kidogo kumbadilisha kwani wakishakuja na watoto basi huwatumia kukuumiza na kukushikilia, ingawa bado unaweza kufanya hivyo ukiamua.

Kama uko katika mahusiano ya kawaida tu, au ni mke wa mtu tayari, sehemu ya pili ya Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” itakusaidia sana kujua namna ya kuweka msimamo, namna ya kumfundisha mwanaume namna ya kukupenda na kubwa kabisa kumfanya mwanaume kukujua, kujua ni vitu gani utavumilia na vingapi huwezi kuvumilia.

Kitabu kinapatikana kwa njia ya Whatsapp, E-Mail au Facebook. Hii ikimaanisha kuwa ukiwa na simu yako au Computer yako unaweza kukipata hapo ulipo ndani ya dakika tano baada ya kulipia bila hata kunyanyua mguu. Kukipata unalipia Shilingi Elfu Kumi (10,000/-) kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 na ukishalipia nitumie SMS Whatsapp au kawaida kwa No. 0742-381-155 kuseama unataka kutumiwa Kitabu kwa njia gani.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA