Usijilaumu kama mtu kakuacha baaada ya Kumgundua kwani angekuacha tu kwa sababu yoyote ile.

 Unakuatana na mtu mnapendana sana, unamuamini anakujali na mnapanga mambo mengi sana, mnatumia muda mwingi pamoja na unaona kabisa kuwa huyu ndiyo mtu sahihi kwangu, anafaa kuwa mke au mume wangu. Lakini katika kipindi cha muda mfupi kunapita upepo flani, wakati wewe ulishajiweka kwake na kufunga milango mingine unakutana na kitu kidogo tu ambacho kinabadilisha kila kitu ulichokuwa unakiamini kuhusu huyo mtu.

man couple love people

Unakutana na meseji moja tu ambayo labda alikosea na kumtumia mtu mwingine au alisahau kuifuta na kuiona kwako kunakufanya kujua kuwa kumbe kila kitu ulichokuwa ukikiamini kuhusu muhusika ni cha uongo. Unajaribu kuongea naye ili angalau kutaka kujua tatizo ni nini, kujua ulikosea wapi labda ukamfanya kuchepuka, ulifanya nini mpaka kufikia hatua ya yeye kukusaliti na kuwa na maisha mengine kabisa.

Lakini pamoja na kwamba kosa ni lake basi anachukulia fursa hiyo ya wewe kujua madhambi yake kubadilika, anaacha kupokea simu zako, anaacha kukujali tena, hajali hisia zako, haombi msamaha wala kuonekana kujutia na sasa ndiyo umempa nafasi ya kuyafanya yale mambo yote aliyokuwa akiyafanya kwa kificho waziwazi. Anaanza kutuma meseji, unakuta picha, anapiga simu na kila kitu anafanya bila kukujali tena.

Unachanganyikiwa, unawaza nimekosea wapi? Mbona kabadilika ghafla namna hii? Wakati mwingine hata unajutia na kujiona wewe ndiyo mwenye makosa kwa kugundua uchafu wake, unajikuta unatamani na kusema laiti nisingejua labda kungekuwa na amani na unadhani kuwa kitendo cha wewe kushika simu yake, kumfumania au kusikiliza maneno mtaani ndiyo kimembadilisha na kumfanya kutokukupenda tena!

Lakini nikuambie kitu jibu ni hapana! Mapenzi yenu yalishaisha zamani na alikuwa anaigiza muda wote, wakati wewe ulikuwa unemuonesha mapenzi yeye alikuwa anakuchezea na angeendelea kukuchezea mpaka siku akichoka anakuacha. Wewe kugundua ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa angalau amekupunguzia muda wa kudanganywa na angalau hata hamkuingia kwenye ndoa kabla ya kugundua, acha kujilaumu, kumbuka si wewe uliyefanya kosa, kumfumania au kujua madhambi ya mwenza wako si kosa lolote hata kama ulikuwa unapekua!

Hata kama ulifukunyua simu yake, hata kama ulikuwa unamfuatilia si kosa lako kujua kwani kama asingekuwa anafanya hayo mambo hata kama kweli umemfuatilia basi usongeona kitu! Usijilaumu kama mtu kakuacha baaada ya kumgundua kwani angekuacha tu kwa sababu yoyote ile hata kama ni ya kijinga namna gani! Mtu wa namna hiyo alishakuacha muda mrefu lakini alikuwa bado tu hajakupa taarifa hivyo acha kujilaumu na kujiona kama vile ni shetani, hujafanya baya lolote kumfumania!


DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA