Je, wewe ni mtu wa kuachwa achwa? Wanaume hawatongozi kuoa wanatongoza Mahusiano

Lengo la kwanza la mwanaume yeyote anapokutongoza kwa mara ya kwanza ni kutaka kufanya mapenzi na wewe. Hilo ndiyo lengo lake la kwanza, mengine huja huko baadaye mbele ya safari.

Asilimia tisini ya anachokuambia mwanaume kabla ya kutembea na wewe ni uongo, ndiyo ni uongo na mara nyingi husema ili tu kukushawishi basi. Sasa dada zangu acheni kudanganyika na wale watu ambao anakuambia anataka kukuoa, hamna wiki kwenye mahusiano kashatangaza ndoa.

basket blur boy child

Kila mwanaume ana rafiki yake mmoja, Dada yake, shangazi au Mama yake mdogo ambaye ni kwaajili ya kutambulishia michepuko yake mipya. Kwamba ili umuamini anakupeleka kabisa kwa Dada yake, sijui shangazi yake au Mama yake mdogo, wengine hata Mama zao wazazi.

Utasikia binti anasema “Mama yake mdogo, shangazi yake, sijui dada yake ananipenda…” Acha kudanganyika huyo ni kazi yake, yaani mpo kama kumi ambao mnapendwa na huyo huyo. Sasa unaweza kuuliza kama ni hivyo nifanyeje?

Unachotakiwa kufanya ni kuwa, ukitongozwa kubali kwakuwa na wewe unataka, jamaa kakuvutia au hata ana pesa atakuhonga au anakuhonga. Kubali kwa sababu yoyote ile lakini si kwasababu ya ndoa, kama unataka ndoa ya mwezi mmoja miwili basi umenoa.

Mwenzako kavumilia miaka minne na bado katemwa wewe hata hajatembea na wewe ushawaza ndoa. Sisemi haiwezi kutokea hapana inatokea, kuna watu hata siku moja tu wanakutana na kuoana lakini usiiwazie, iache itokee kama miujiza huku ukila raha. Unapolazimishia umetongozwa tu ushajivalisha shela basi baada ya muda unaanza kuboa na unajikuta unakuwa mtu wa kuachwa achwa!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA