HII NDO INAITWA S M A R T D A T I N G .
Mahusiano si kuwa na Boyfriend handsome au kuwa na msichana mzuri. Si kutafuta mtu aliyekamilika kwa sababu hakuna aliye mkamilifu duniani.
Sio kutafuta mtu aliye tajiri kwa sababu pesa hainunui mapenzi, bali mapenzi ya dhati huwa chachu ya kuleta pesa...!
Mahusiano ni kutafuta mtu ambae atakuheshimu, atakaekujali, kukulinda, kusimama na wewe katika hali yoyote ile..mwenye kukutia moyo pale unapohisi unashindwa jambo fulani na kukata tamaa... atakaekuelewa, atakaejivunia kuwa na wewe, na atakaekupenda jinsi ulivyo.
Ambae atakuwa muaminifu kwako, mwenye kukufariji. Yule ambae atakuvumilia bila kukata tamaa licha ya magumu fulani unayopitia
Watu kama hawa ni nadra sana kuwapata siku hizi hapa duniani kwa maana mchezo huu umevamiwa na wachezaji wasiojua kanuni na taratibu za huu mchezo.. Wanacheza rough hakuna fair hata kidogo kwakuwa wanachojali ni kukidhi haja na matamanio yaoo, na si mioyo ya wenza wao.............
Hivyo basi kama umebahatika kuwa nae mtunze vizuri, shikamana nae kwa umakini zaidi, uwe mwaminifu na umpende kweli bila ya kumuumiza kihisia kum-let down.
Kama hauna mahusiano kama hayo, endelea kumuomba Mungu huku ukijitunza vyema. Mungu atakujalia na utapata mtu wa aina hiyo, muda wako utakapotimia, kubwa usiwe na pupa ya mahusiano, ukaishia kuumia.. Mungu anakuandalia mtu aliyebora kwako.. Magumu unayopitia sasa ni daraja la kukuvusha na kukujenga kiimani na jinsi ya kukabili maumivu yako.. Amini kuwa kuna mtu ameibeba furaha yako ya maisha aliyopewa na Mungu. Mungu anamjua na amesha muandaa, muda ukifika atakupatia na utafurahi sana..
"Good relationship is knowing someone's weekness, and not taking advantage of them. Knowing their flaws and accepting who they are."
@maisha_halisitz