Kama unafanya hivi basi jua kuwa unajitengeneze Mateso wewe mwenyewe!


Moja ya vitu ambavyo huwezi kufanya na ukafanikiwa ni kulazimishia mapenzi, hakuna namna unaweza kumlazimisha mtu akakupenda pale anapokuchoka na kwa bahati mbaya jinsi unavyopzidi kumlazimishia mtu kuwa na wewe ndiyo jinsi unavyozidi kumpoteza.
Kuna watu kiasilia hawakubali kuachika, hawakubali kuambiwa sikutaki, kwao ni kama dharau, ni kama kusimamisha maisha yao. Kwa wanaume hii inaweza kuwa na unafuu kidogo, kwamba mwanaume unaweza kujilazimishia kwa mwanamke kwa muda mrefu kidogo na mwisho mwanamke akaamua kubaki na wewe.
Mwanamke anapokosa mtu mwingine kuna wakati anasema basi bora kubaki na huyu. Lakini kwa mwanamke kujilazimishia kwa mwanaume ni kufungua mlango wa mateso. Iko hivi, ni wanaume wachache sana ambao watakukataa pale ukijilazimishia kwao, kwa mfano, labda mwanaume amekuacha, ana mtu wake, labda kaoa au ni mpenzi wake tu.
Kama ukijilizaimishia kwake kwakua unasema unampenda basi huyu mwanaume anaweza asikuache, ataendelea kufanya mapenzi na wewe lakini hatakua mpenzi wako. Wewe ndiyo utakua unapiga simu kila dakika, ataendelea kuongea na wanawake wengine mbele yako bila kujali, atachukua pesa zako na mwisho kama ukizaa utaishia kulea mtoto mwenyewe.
Yeye hatajali na baada ya muda utajikuta umepoteza muda mrefu kwa huyo mwanaume nusu kuchanganyikiwa. Mwanaume anapokuambia sikutaki, anapokuambia kuwa hahitaji kuwa na mapenzi na wewe ni wakati wa kurudi nyuma kidogo, jipe muda wa kujifikiria hivi na mimi namtaka au ni upweke unanisumbua. Achana naye kwa muda kwani mara nyingi utajikuta unang’angania mtu ambaye hata hakua na maana kwako.
May be an image of 1 person, standing, sunglasses and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA