WADADA AMBAO MLIAHIDIWA NDOA MKIWA CHUONI HEMBU TUPENI UZOEFU WENU!


Mimi ni Binti wa miaka 21, nipo chuo mwaka wa kwanza, naomba ushauri wako, nina mchumba wangu ambaye mwaka huu mwezi uliopita alinivalisha Pete, nampenda na mimi ananipenda, kila kitu tunafanya pamoja na kila mtu anajua kuwa huyu ni mpenzi wangu.
Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, huyu mpenzi wangu ana wivu sana, yaani hataki niwe na mazoea na mwanaume mwingine yoyote, mimi na yeye tunasoma kozi tofauti, kama unavyojua kuwa darasai ni lazima kufanya assignment na tumepangwa magroup ambapo mimi nimepangwa na wakaka wa tatu wadada nao tuko watatu.
Sasa kaka hataki kabisa mimi kushiriki nao, ananoapangia muda wa kuonana na kuna Kaka mmoja ambaye ni kama kiongozi hampendi, ameniambia nihakikishe kuwa natafuta group la wanawake tu na kama siwezi ni bora tuachane. Nimemuomba msamaha lakini hataki kunielewa ameniambia kuwa nichague kati ya hilo group au yeye.
Nilaimua kuacha kwenda kwenye discussion lakini naona kwenye test nafeli kwani sina mtu wa kusoma naye. nina rafiki wa kike lakini nao hawataki kusoma sisi peke yetu wkakau kuna mambo mengi hawayajui hivyo nahangaika tu mwenyewe chumbani na kwakua tunasoma kozi tofauti basi nashindwa kusoma naye.
Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, jana nilimuomba sana kuwa niwe nafanya discussion na wenzangu akaniambia atanikubalia kwa sharti moja kwamba nibebe mimba yake kwani nikiwa na mimba ndiyo siweiz kuchepuka na kumuacha. Yuko tayari kuja kwetu kujitambulisha kwani ananipenda sana na mimi nampenda, tuko naye mwaka mmoja ila yeye ni mkubwa kwangu ana mika 22, naomba ushauri wako Kaka nifanye nini?
May be an image of 1 person, standing, footwear and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA