KUWA KATIKA MAHUSIANO YA MUDA MREFU HAIMAANISHI ANAKUPENDA SANA

Nadhani hili ndiyo la muhimu zaidi na hapa ndiyo nataka uamke. Kwama mwanaume hajakuambia nitakuoa basi acha kujiozesha mwenyewe eti kwakua mko kwenye mahusiano muda mrefu.
Sisemi kwamba hatakuoa lakini nasema kua hembu fungua macho, kuna sababu nyingine zaidi ya hiyo. Inawezekana kweli anakupenda na anampango wa kukuoa lakini pia inawezekana pia yuko na wewe muda mrefu kwa sababu hizi;
Kwanza labda yuko na wewe kwa muda mrefu wakati akitafuta mke wa kuoa. Kwamba wewe ameona kabisa unafaa kwa matumizi ya wakati huo lakini hana mpango hata wakukuoa. Pili inawezekana hata hauko peke yako.
Inawezekana umekua naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu ukadhani kua labda anakupenda sana kumbe kuna mwenzako wako kwenye mahusiano kwa miaka mitanpo na mwingine miwili na wote kama wewe washajiahidi ndoa.
Yaani wote kama wewe ashawatambulisha kwa marafiki zake, lakini haiishii hapo hata nyumbani wanawafahamu, kua wameshampeleka nyumbani kwao kama ulivyompeleka wewe na kwapo kaishia kukupeleka kwa yule mdogo wake wakike.
Ndiyo kuna yule mdogo wake wakike anakuita wifi kila siku, yeye anawajua wote na wote anawaita wifi kama wewe. Lakini jambo la tatu inawezekana kweli anampango wa kukuoa lakini kumbe hajakutana tu na mke wake.
Kwamba mkiwa kwenye maandalizi akakutana na mwingine akamteka kabisa na ndani ya miezi mitatu wanaoana wakati wewe ulishavumilia miaka mitano. Lengo langu hapa sio kukukatisha tamaa bali kukuamsha kutoka usingizini.
Hembu furahia mapenzi sasa na acha kujiahidi ndoa kisa mmekaa muda mrefu. Eti kwakua una uhuru wa kwenda kwake wakati wowote ukajiona Mama mwenye nyumba, sasa wewe unaenda kwake uko huru kuna wenzako wamepangiwa nyumba kabisa.
Lakini inawezekana unaenda kwake na wadada mlivyo eti unaacha vinguo vyako vya ndani, taulo lako, khanga na visendo vyako ili mwanamke mwingine akija aone kua ana mwanamke. Dada zangu hivi mnafikiri sisi ni wajinga kiasi hicho.
Yaani ile unaondoka tu jamaa anaviochukua anaweka kwenye box na kuficha uvunguni au darini, akikuambia njoo anavitoa na kurudisha ulipoviweka. Lakini kuna wanawake wengine wala hawajali, anakuja na tena anatumia khanga yako hiyo hiyo.
Kwani bei gani? Anajua wako zaidi ya mmoja na hajali halafu kwa taarifa yako sasa hawa ndiyo unakuta wanaolewaga kwani si wasumbufu sana, tofauti na wewe ambaye kila ukifika unaanza kukagua kila kitu!
Ujumbe wnagu hapa nikua acha kujiahidi ndoa kwasababu ya muda, kama ndoa inakuja ije tu. lakini pia acha kumuamini mwanaume asilimia mia, sisiemi usimuamini kabisa bali hembu fanya mambo yako ya maendeleo.
Ndoa ikukute unakiwanja chako, ushajenga kwako, unabiashara yako. Lakini haya mambo ya kumuamini, ukawekeza naye, mrtu si mume wako mnafungua biashara ya pamoja, mtu si mume wako mnajenga pamoja, mtu si mume wako unamchukulia mkopo!
Dada yangu utaishia kutoa laana tu kua eti kwakua kakupotezea muda na kaoa mwingine Mungu atamuona. Sasa dada yangu wewe unalalamika kakupotezea muda mnna miaka mitatu sasa na yule wa miaka mitano asemeje?
Kwanza mlikua mnafanya dhambi kipindi chote hicho halafu unasema unamkdbishi Mungu. Kuachwa namna hiyo nisawasawa na mmetoka kuiba mkavunja nyumba ya watu halafu baada ya kuiba mwenzako akakudhulumu mlichoiba halafu mnamkabidhi Mungu.
Ndiyo mlikua mnaiba kwa kuzini na kufanya majukumu ya mke wakati wewe sio mkewe, hiyo ni dhambi kwa dini zote hivyo hembu acha kuendelea kukufuru kwakua eti kaacha kufanya dhambi na wewe kaamua kumrudia Mungu na kuoa mwingine!
Furahia tu dhambi hiyo furahia mapenzi lakini wekeza kwako, kama ni kujenga muambie Baby najenga kwanza halafu ukishanioa ndiyo tuachanganya nyumba, Baby nafungua bishara yangu halafu ukinioa tutachanganya na yakwako.
Acha kuwa mjinga na kumuamini mwanaume kirahisi rahisi namna hiyo, hivi jiulize kwani akikuoa ukiwa una nyumba yako ndiyo hiyo nyumba itageuka kichuguu au akakuoa ukiwa na biashara yako itapunguza nini mpaka ujipe kiherehere ch akumpa mtaji au kumuongezea ajenge.
4

May be an image of 1 person and text that says "PHOTOGRAPHIE"

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA