USIRUDIANE NA MPENZI WAKO MLIYEACHANA ETI KISA KAKUAMBIA "AMEBADILIKA"


May be an image of 1 person and sunglasses
-Unapotaka kurudiana na mpenzi wako,usirudiane nae kwakua kabadilika,huwezi kupima kubadilika kwa mtu hata siku moja.
*Anaweza kubadilika kwa maneno.
*Akabadilika kwa muda au akaigiza kubadilika.
Mtu pekee unayepaswa kuangalia kama kabadilika au la ni wewe mwenyewe.
Badala ya kuwaza**je ataninyanyasa tena**basi waza akininyanyasa tena nitafanya nini? Badala ya kuwaza**je ataendelea kutoka nje ya ndoa**
Basi waza je akitoka nje ya ndoa nitafanya nini? Ni lazima uwe na majibu ya hayo maswali na kama huna hayo majibu basi ni kazi bure hata ukirudi.
Rudi kwakua umebadilika,umekua mtu mpya,hunyanyasiki na wala hupigiki tena, lakini kama unarudi huku ukiwaza je kabadilika kweli au la!!!
Basi acha usirudi,kwani kubadilika kwa mtu ni kati ya mtu mwenyewe na Mungu wake.
Hatua ya kwanza ya wewe kubadilika ni kujipenda wewe,kutambua kuwa maisha yako yanathamani,kutambua kuwa furaha yako ni ya muhimu na haipaswi kumtegema mtu yoyote yule.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA