KAMA NDIYO UMEMALIZA CHUO BASI JUA KUA HAKUNA MILIONI 10 ZINAKUSUBIRI MTAANI!

Kama ndiyo umemaliza chuo unatakiwa kujua kua hakuna milioni kumi ambazo zinazurura mtaani na kukusubiri wewe ili uzifanyie biashara. Unatakiwa kujua kua hakuna mzazi ambaye atahangaika kukulipia ada, atakopa na kujinyimka ili usome halafu urudi umuambie nipe na milioni kumi nikafanya biashara na kama wapo ni wachache sana!

Kwa wazazi wengi kusoma inaamanisha kuajiriwa na kama utamaliza chuo bila ajira inamaanisha umeshindwa maisha, kwa maana hiyo kama kijana ni lazima ujiongeze wewe mwenyewe, ni lazima uache kusubiri milioni kumi ndiyo ufanye biashara ya kisomi na kuabdilisha hiyo elfu kumi au laki moja ambayo ni rahisi kwako kuipata na kuifanya kuwa milioni kumi.

Kama huwezi hivyo basi miaka mitano baadaye utakua umekaa sehemu unalalamika kua ajira hamna na utakutana na watu wengi wa darasa la saba ambao wana biashara zao na ukiwauliza walianza na mitaji kiasi gani watakuambia elfu kumi mpaka laki moja ambayo kwa wakati huo utakua huna au unayo lakini umri nao utakua umeenda.

Sikuambii nirahisi kihivyo, hapana ni ngumu, sikuambii hutaona aibu hapana utaona sana kwani biashara ya mtaji namna hiyo nilazima uanzie chini lakini mwisho wa siku ni bora kuanza leo kuliko kusubiri kesho. Kama unatamani kuanza biashara na hujui nini cha kufanya hembu soma Kitabu changu cha “Biashara 50”.

Kuna mifano 50 ya biashara ambayo unaweza kuifanya ukiwa na mtaji kidogo, kumbuka Kitabu hakikufundishi namna ya kufanikiwa bali namna ya kaunza biashara, kufanikiwa katika biashara ni mchakato mwingine kabisa ambao unakuhitaji wewe zaidi kuliko kusoma Kitabu. Anza sasa, jifunze na ukikwama nipigie simu tuongee.

Kupata Kitabu hiki unalipia Shilingi elfu kumi kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 baada ya hapo Kitabu unatumiwa kwa njia ya Whatsapp, Facebook au Email na kukisoma kupitia simu yako au Computer, hakuna Kitabu cha karatasi. Hakuna kitu kitabadilika katika maisha yako kama hutachukua hatua sasa na kulalamika si sehemu ya hizo hatua.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA