ACHA KUMLAZIMISHA AHISI UNACHEPUKA ACHA KUFICHA KAMA HUNA CHA KUFICHA!

MTEJA; Kaka mimi mume wangu ananisumbua anataka kushika simu yangu wakati mimi si shiki yakwake. Nimeweka password ila anakasirika yaani sijui hata nimfanye nini huyu mwanaume.
IDDI MAKENGO; Kwanin kuna ubaya gani mume wako kushika simu yako, si mume, unaficha nini mpaka hutaki ashike, unachepuka?

MTEJA; Hapana lakini kaka si ulisema kuwa kila mtu anatakiwa kuhangaika na simu yake na si mambo ya kuchunguliana kwenye simu.
IDDI MAKENGO; Hapana, hukunielewa vizuri, nilisema hivii “Kama huna ubavu wa kumuacha mpenzi wako usiguse simu yake!” mume wako kuamua kushika simu yako inamaana yeye anajua kabisa kama akikuta madudu hataishia kulia na kuomba msamaha yeye anaweza kukurudisha kwenu na maisha yakaendelea.

MTEJA; Lakini kaka mbona kama unawatetea wanaume kushika simu za watu.
IDDI MAKENGO; Hapana dada, hata wewe unaweza kushika simu yake. Lakini utakayoyakuta huko basi unamaamuzi umuache au unyamaze na kisirani chako, lakini sio ushike, ukute madudu halafu umuambie aombe msamaha hapana utakua ni msamaha wa uongo tu na hautakusaidia kitu. Kama unajua kabisa ukifumania huwezi acha, basi achana na simu yake.

MTEJA; Kwahiyo Kaka unanishaurije?
IDDI MAKENGO; Mume wako anaonekana ana ubavu wa kukuacha kama akikufumania. Kwa maana hiyo muache ashike simu yako na kama una madudu yako achana nayo. Pili kama ukimzuia kushika simu yako inamaana ni kama kuna kitu unaficha na mume wako hata kama huchepuki ataamini unachepuka. Kama huna chakuficha kwanini uhangaike na kufichaficha mpaka mtu akuhisi unachepuka, acha haikusaidii kitu!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA