BOSI WANGU ANANITAKA KIMAPENZI NIFANYE NINI NA MIMI NINA MCHUMBA?


Habari Kaka mimi ni binti wa miaka 27, sijaolewa ila niko wkenye mahusiano na mpenzi wangu huu ni mwaka wa nne. Ninafanya kazi katika kampuni moja ya ujenzi, sasa hapa kazini kuna Bosi wangu ambaye ni mmoja wa wamiliki wa hii kampuni, wapo wanne ila huyo ninayemzunguimzia ndiyo anasimamia sana.

Sasahuyu Baba ni ananitongoza, ananisumbua kiasi kwamba anaweza kunipigia simu mpaka usiku, sasa boyfrienda wangu anakasirika na kudhani labda nipo kwenye mahusiano naye. mimi siko kwenye mahusiano naye kwani ni mtu wa wanawake, anatembea na karibu kila mwanamke anayefanya kazi, namjua na ninamkwepa.

Lakini shida Kaka ni hivi, naona kama nisipomkubalia nitapoteza kazi yangu kwani huwa ana kawaida ya kuwafanyia figisu mpaka kufukuzwa kazi. Kwenye mahusiano yangu mchumba wangu naye haeleweki, kila nikimuambia suala la ndoa ananiambia kuwa nisubiri kwani bado anajipanga, sasa Kaka nahofia kama naweza kumkataa Bosi nikilinda penzi ila mwisho wa siku bado nikaachwa, naomba unisaidie nifanye nini Kaka?

IDDI MAKENGO; ACHA KUFANYA MAAMUZI KWA KUWAANGALIA WANAUME

Katika maisha yako usifanye kitu kwa kumuangalia mtu, kama unamkubali Bosi wako basi umkubali kwakua unamtaka, unataka umdange au kwakua tu mvua inanyesha. Lakini kama unamkataa basi mkatae kwakua wewe ni binti, unajiheshimua na huwezi kushusha thamani yako kwajili ya kazi.

Ukimkataa Bosi wako kwakua una mwanaume unahisia takuoa na si kwakua una akili unajilewa basi hata hayo mahusiano yatakufa kwani kwakua umemkataa utahisi mwanaume wako ana deni kwako, asipopokea simu utawaza nimemkataa flani kwaajili yake ila hapokei simu zangu, asipokupa pesa utawaza nimemkataa flani kwa ajili yake lakini hanipi pesa.

Yaani kila kitu utakua unajutia ukilinganisha kuwa ulimkataa Bosi wako wkaajili yake mwisho utakua na kisirani cha ajabu mtaishia kuachana. Bosi wako ni malaya, wanaume malaya kama huyo akitembea nawewe anaishia kukuhonga bia na viout vya kijinga jinga kisha anahamia kwingine. Wewe unakua umeuza utu wako, umekua kama umejiuza kwake.

Kwa maana hiyo kama sio tabia zako achana naye kwani mwisho wa siku utaishia kujichukia mwenyewe. Sijui kama mchumba wako atakuoa, lakini ninachojua kwua kama ameshaanza kukuhisi kuhusu Bosi wako sikua kigundua basi itakua mwisho na hata isipokua mwisho bado hamtakua na amani, kataa kwakua unajiheshimu sio kwakua una mchumba.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA