WATOTO WACHUO AMBAO MNADHANI MNAYAJUA MAPENZI KULIKO SISI WAKONGWE!


Watoto wa chuo naomba niwaambie hivi, tunajua mnafanya mapenzi kweli lakini acheni kujiozesha. Hao wanafunzi wenzenu mnaotembea nao na kudanganyana kuhusu ndoa hawajajua kutafuta pesa, siku wakiingia mtaani maisha yakwapiga watasahau hata majina yenu.

Kwa maana hiyo hembu wakiwaambia kuhusu kuzaa, sijui nakupenda, nipo tayari kufa kwaajili yako, wakikuambia ujinga kama beba mimba nikimaliza natafuta kazi waambieni kwaheri maana kazi hazipatikani kirahisi namna hiyo.

Lakini nyie mnaotembea na waume za watu aisee hawawaachi wake zao. Mnaweza kujiona kama keki sasa hivi mkafikiri wake zao ni wajinga, hawajui mapenzi, hawajui kumhandle mume ila si kweli. Mnadanganywa, mkibeba mimba zao wanarudi kwa wake zao, kuna toafuti kati ya kununua bia na kununua Pampas.

Kuna wale ambao mko kwenye mahusiano na vijana hawajaoa wana kazi zao mtaani. Nyie ndiyo mnaona ndoa hizi, wadogi zangu, watuw ana watu wao lakini hata kama hawana hembu punguzeni kudhani kama mnayajua mapenzi sana, mkabeba na mimba kisa mmeahidiwa ndoa, aisee nyie watoto mna kasi sana mpaka mnaboa.

Yaani mnahdani mambo ni rahisi tu kwakua mshikaji ana kazi basi ukimaliza chuo anakuoa. Subiri kwanza ingia mtaani, ndiyo ndoa ije, subiri kwanza ndoa ije ndiyo ubebe mimba. Hizi mambo za uko mwaka wa mwisho beba mimba ukimaliza nakuoa unajifungua achana nazo kabisa!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA