MAMBO 5 YA KUWAAMBIA WANAWAKE WENYE KIPATO PALE TU WANAPOINGIA KWENYE NDOA

(1) Hamuwezi majukumu ya kuhudumia familia hivyo msijaribu; Mwanamke hata awe analipwa milioni mia kwa siku lakini hawezi kubeba majukumu ya mwanaume kama vile kulisha familia, kulipa kodi, kusomesha watoto na vitu kama hivyo, atafanya kwa muda ila atachoka na kulalamika.

Mwanamke anatakiwa kuchangia, hata kama anatoa kikubwa lakini anapaswa kuchangia kwakua wanawake wanachoka, akihudumia familia kidogo tu anahisi kama kabebeshwa mzigo wa mawe hivyo kuichoka ndoa mapema, kwa maana hiyo ukiingia kwenye ndoa tu, muachie mume wako majukumu yake kwani yatakushinda tu.

(2) Muache mume wako awe mwanaume mwanzo tu wa ndoa; Muache mume wako awe mwanaume, yeye ndiyo aamue kuwa mtaishi wapi kwa maana kulipa kodi au la, aamue watoto watasoma wapi na apange mambo yote. Hata kama umemzidi kipato lakini ni wajibu wake yeye kama mume kupanga hayo mambo, mwanzo kabisa wa ndoa usiwe na hataka ya mafanikio na kulazimisha mambo ambayo mume wako hana uwezo nayo.

(4) Msaidie mume wako kwa kuongezea baada ya kuongea naye; Najua kuna wanawkae wamebarikiwa kuwa na pesa kuliko wanaume na wakati mwingine unakuta mwanaume wako hana kazi kabisa. Bado usiwe na mwanaume, msaidie lakini baad aya kuongea naye, yaani usifanye maamuzi huko na kuja kumpa mume wako taarifa kwakua tu hana pesa.

Kwa mfano, wewe ndiyo una pesa ya kulipia kodi mume wako hana au ana pesa kidogo amabyo haitoshi nyumba mnayoitaka. Badala ya kutafuta dalali na kulipia nyumba kisha unamfuata mume kumuambia muhamie, ongea naye kwanza muulize kama anataka hiyo nyumba, kama anataka basi aitafute yeye na katika kulipia basi alipie yeye.

Hata kama pesa ni yako lakini mwanaume ndiyo aongee na mwenye nyumba inamaan akodi ikiisha adaiwe yeye na si wewe. Unataka kununua gari, una pesa yako, ongea na mume wako muelewane kwanza, na kama haiwezekani kwa wakati huo basi acha na fanya kingine, sio umpe hela aandike kila kitu jina lake labda nyumba na gari kwakua yeye ni mwanaume? Hapana ila kama mume wako ongea naye ajue unafanya kitu gani.

(5) Ndugu zako si sehemu ya ndoa yako; Unapokua umemzidi kipato mume wako ndugu zako wanaweza kujiona kama ndiyo kila kitu, mamauzi yanafanyikia kwenu mume anapewa taarifa, mnapanga vitu kwenue yeye anaalikwa tu au hata kuambiwa haambiwi.

Labda nyumba ni yako ndugu zako wanakuja na kujioachia kama kwao, hapana. Umeoelwa mume wako ndiyo kicha cha familia, jadili mambo na mume wako na fanya mamauzi nayo, hata kama ni mawwazo ya ndugu zako au ni maamuzi ya ndugu zako lakini jadiliana na mume wako kwani yeye ndiyo familia yako.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA