Wanaume ;MBINU ZA KUONGEZA FURAHA KWENYE NDOA YAKO




1. Rejesha mahaba yako kwa kumwambia mkeo “Nakupenda”, sema hivyo angalau mara moja kwa siku. Neno hilo linaweza kuwa na athari kubwa kwake.

2. Ndoa yenye furaha inatengenezwa na dhamira ya kujitoa (commitment), urafiki wa dhati, kujuana vizuri, kuheshimiana, kujua wakati muafaka wa kushughulikia jambo.

3. Yakupasa kuwa mwema kwa mkeo. Fanya mambo madogo madogo, lakini yafanye mara kwa mara na kwa moyo wa dhati. Vitu vidogo vidogo huwa vinafanya maajabu na kuwavutia wanawake.

4. Licha ya mamlaka uliyonayo kwa mkeo na familia yako, tafadhali, usiitumie vibaya haki hii. Usimtenge mkeo kabla hujafanya juhudi zote kumrejesha mkeo kwenye msitari.

5. Kukaa pamoja na familia yako inatakiwa kuwa kipaumbele chako, kabla ya marafiki. Mkeo na wanao wanapenda ukaribu wako na watakushukuru na kukuthamni iwapo utatumia muda wa uhuru wako kushirikiana na kukaa nao.

6. Msiende kulala mkiwa mmekasirikiana. Jaribu kutatua tatizo haraka iwezekanavyo na kwa utashi wa dhati. Usiombe msamaha halafu ukabaki na kinyongo. Kuna wengine wakati wa kuomba msamaha husema: “Basi nisamehe, lakini nawe una makosa. Ulitakiwa kufanya hivi na hivi…” Omba msamaha kwa moyo wote. Samehe na usahau hata kama unahisi kwamba mwenzako ndiye aliyekuwa na kosa.

7. Jtahidi sana kadiri uwezavyo kumsaidia kazi ndogo ndogo za nyumbani. Pia usimchoshe kwa kazi anapokuwa hajisikii vizuri.

8. Mletee zawadi mara kwa mara, hata kama ni ndogo. Usisubiri matukio maalumu. Ukubwa wa zawadi sio muhimu, bali moyo wa mahaba uliobebwa ndani ya zawadi hiyo. Zawadi na usafi ni miongoni mwa vitu vinavyoimarisha sana mahaba.

9. Jitahidi sana kutomfokea au kumdhalilisha mkeo mbele ya watu wengine, au kumlinganisha na wanawake wengine kwa namna ya kumshusha. Kadhalika, usitumie maneno makali au yenye ukakasi unapozungumza nae hata kama umekasirika.

10. Wanaume wengine hupenda kuwadhihaki na kuwatukana wake zao pale mtu wa upande wa mke anapokosea jambo. Tabia hii mbaya inaweza kuchafua hali ya hewa baina ya wanandoa.

11. Angalia kwa makini zaidi lugha unayotumia ukiwa nyumbani. Lugha mbaya, matusi na maapizo kutengeneza mazingira mabaya nyumbani acha hivyo

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA