NINI CHA KUFANYA; MUME WANGU AMENIACHA KWENDA KUISHI NA MAMA MTU MZIMA!


Habari Kaka iddi, mimi ni Mama wa miaka 33, nimeolewa miaka nane sasa, mume wangu alipata mwanamke mwingine, Mama mtu mzima akwa ana mahusiano naye, nilipogundua aliniambia ananipenda mimi na huyo Mama anakua kama anamchuna tu, alinisihi sana nisimuache niliamua kuvumilia kwakua na mimi sina kazi na namtegemea yeye.
Lakini ghafla mume wangu kahamia huko moja kwa moja, hahudumii watoto na nikimuambia anakasirika ananiambia nina mikono nikasukume chapati, hataki kunipa mtaji, kaniachaia watoto watatu nalea mwenyewe. Wamefunga ndoa ya serikali wakati tuna Ndoa ya Kanisani, nahisi mume wangu kalogwa si akili zake!
JIBU LANGU; Mume wako kafuata pesa hakuna kulogwa hapo! Kitu pekee kinachowapa amani ni usumbufu wako. Akiwa kwa huyo Mama wanakuongelea wewe, wanaongelea namna unavyolalamika, wanaongelea unavyosumbua ndugu zake kutaka waongeee naye, wanacheka wanafurahi, wanalala!
Najua ni ngumu, lakini kama utaamua na kusema, huyu mwanaume sikuzaliwa naye, nilikua naishi kabla ya kuwa naye na sasa hivi nitaishi baada yake. Ukachukua suhauri wake, una mikono, ukasukuma chapatti, niamini nikikuambia kuwa, wakikuona una amani husumbui basi kuna mambo mawili yatatokea;
(1) Mwanaume atahisi una mwanaume mwingine anakuweka mjini, kwakua bado anakupenda, atakua hana amani, ataanza kukufuatilia. Atakua na kisirani na kwakua wewe utakua unajipa raha mwenyewe, hasira zako umepeleka kazini basi kisirani atahamishia kwa huyo Mmama wake.
(2) Mwanamke akikuona kimya husumbui, ataanza kupost status, kurusha vijembe, kupiga kelele, kwakua unanisoma hutamjibu wala hutalalamika kwa mwanaume wako, basi atapaniki, ataamini kuwa hulalamiki kwakua umerudiana na mwanaume, mna furaha, atakua na kisirani na wataachana au hawatakua na amani.
Ukifuata ushauri wangu, ukawa na amani, unafanya mambo yako, huyo mwanaume hamalizi mwaka na huyo Mama. Ila muhimu si wao, muhimu nikuwa, huo mwaka akirudi akute una kitu flani, thamani yako imepanda. Atakuheshimu wewe, ukoo wako na hata Inzi wa huko kwenu atawaheshimu.
Acha kulia kasukume chapatti njoo leta mrejesho! Lakini kama ukiendelea kulialia inamaana ni kama unamuambia mwanaume siwezi kuishi bila wewe. Hapa hata kama mwanaume anakupenda lakini hajali wala kukuheshimu tena kwakua anajua huendi popote, anajua kuwa wewe ni wa kumtegemea yeye tu!
May be an image of 1 person and text that says "Habari Kaka iddi, mimi ni Mama wa miaka 33, nimeolewa miaka nane sasa, mume wangu alipata mwanamke mwingine, Mama mtu mzima akwa ana mahusiano naye... IDDI MAKENGO CEO AZIRANI MAGAZINE www.azirani.co.tz www. @Aaziranimagazin @Aaziranimaga f"

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA