MAMBO 5 YA KUYAJUA UNAPOCHEPUKA NA MUME WA MTU AMBAYE ANADAI MKEWE ANAMTESA!


(1) Kugombana si kuachana hivyo hata kama hawapatani namna gani basi jua kuna uwezekano wa kurudiana hivyo usimpe maisha yako yote. Unapoamua kumfanyia vitu kama kumzalia mwanaume huyu, kumpa mtaji kwaajili ya Biashara, kununua kiwanja na kujenga pamoja na mwanaume wa namna hii, kumuamini na kuachana na mpenzi wako kwaajili yake basi jua kuwa unacheza patapotea. Kama hajamuacha mke wake basi bado anampenda.
(2) Wanaume wengi wanaoanzisha mahusiano ya nnje ya ndoa kwa kuwashutumu wake zao, kuongelea tabia mbaya za wake zao basi mambo mengi ambayo anakuambia basi ni yeye anayafanya. Inawezekana mwanamke wake akawa ni mkorofi lakini ni kwakua amechoka tabia zake, wanaume wengi wanaonyanyaswa na wake zao hawasemi kwani huona aibu, wao hupenda kujisifia kua wao ndiyo hutesa ila ukweli ndiyo huteseka, ukisikia anajisifia kuteseka basi kua makini mara mia.
(3) Kama ameoa kwa maana kafunga ndoa na huyo mwanamke hata kama anakupenda namna gani na anakushirikisha kwa kila kitu lakini kisheria yeye ndiyo mke wake na huyo mwanamke ana haki zote kama mke. Vitu vyote mnavyochuma na huyo mwanaume kama vina majina ya mwanaume hata kama wewe ndiyo umetoe kiasi kikubwa cha pesa basi kisheria mke wake ana haki navyo na wewe huna haki zozote.
Kwa mfano, kama mmejenga nyumba, lakini kiwanja kina jina la huyo mwanaume. Kisheria kama hawajapeana Talaka ya mahakamani na mke wake basi jua kuwa, akifa nyumba ni ya mke wake huchukui kitu, wakitaka kudai Talaka mahakamani mwanamke yule hata kama hatapata nusu kwa nusu ila ana haki, akitaka kuiuza mkewe anaweza kuweka pingamizi na kama ana wakili mzuri akashinda ila wewe huna haki yoyote ile.
(4) Watoto mliozaa naye wanatambulika kama watoto wa Kimada (sio tusi). Kama akifa hawarithi chochote hata kama mlichuma wote, ili watambulike kisheria mwanaume anapaswa kuwatambua, kuna namna nyingi za kuwatambua, kwanza Kuacha wosia, Mahakamani, kuwakatia bima kama watoto wake, kupeleka Document kazini kwake na kama si mfanyakazi basi aende kwenu kutoa faini ya kimila na kuwe na mashahidi torfauti na hapo sharia inawatambua kama watoto wa Kimada na huwa hawarithi kama hakuna wosia.
𝐙𝐈𝐍𝐆𝐀𝐓𝐈𝐎; Ingawa nimetaja njia nyingine za kuthibitisha lakini Sheria inasema kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa anaweza kuhalalishwa kwa kufuata taratibu za mila na desturi za jamii husika na hatimaye kuwa mtoto halali ambaye anaweza hata kurithi.
Kwa maana hiyo ni vyema kama ikitokea umezaa na mwanaume nnje ya ndoa (hata kama hajaoa) basi mhalalishe kimila, kwamba aje hata kwenu na kutozwa faini kulingana na kabila lenu ili kujiweka vizuri zaidi. Hizo njia nyingine kama kuna ubishani basi mara nyingi unahitaji Wakili mzuri ili kushinda.
(5) Kama mwanaume ametengena na mke wake, au bado wanaishi pamoja lakini hapatani na mke wake, akakupeleka kwa ndugu zake wakajifanya kukupenda sana, kila dakika wanampondea huyo mwanamke mwingine na hata kufanya vitu vya kumuonyesha mke wa Kaka yao kuwa Kaka yao anachepuka na wanampenda huyo mwanamke mwingine basi hakuna upendo hapo.
Ndugu wanamchukia huyo mwanamke mwingine kwakua wanadhani anakula pesa za Kaka yao na wanajifanya kukupenda ili kumkomoa. Ukifanikiwa kuingia kwenye hiyo familia basi watakugeuka kama hutafuata matakwa yao hivyo kua makini na usiingie kichwakichwa mwenzako ananyolewa usipotia maji watakung’oa nywele.
May be an image of 2 people, people standing, flower and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA