CHEKELEA LAKINI SIKU WAKIACHANA HATAKUA NA AMANI MPAKA ADHALILISHE MTU MWINGINE

 




Katika mahusiano mara nyingi ni nadara sana kukutana na mtu ambaye hajawahi kuwa na mtu. Tena wakati mwingine unaweza kuingia kwenye mahusiano na mtu wa mtu kisha akawa mtu wako. Wakati mwingine hata ukajikuta unaingia kwenye mahusiano na mume au mke wa mtu mkapendana na hata mhusika kumuacha mume au mke wake.

Bila kujali sababu zao za kuchana lakini kama unataka kuwa na amani na huyo mtu basi kamwe usifurahie mateso ya mtu mwingine. Kama una mpenzi lakini kila siku akiwa kwako anamuongelea vibaya mpenzi wake wa zamani, anakuambia umpigie simu umtukane, anakuruhusu umtumie meseji za matusi na picha za ajabuajabu ili tu kumuumiza.

Anampiga na kumtukana mbele yako huku akikusifia wewe na madudu mengine mengi mengi basi jua kuwa hata ukimpata huyo mtu ipo siku yatakugeukia. Unampenda sawa na pengine huwezi kumuacha lakini acha kufurahia ujinga wake kwakua tu anafanyiwa mwenzako, kumbuka siku huyo mwingine akiondoka basi utafanyiwa wewe huo ujinga.

Akikupa namba yake ili umpigia mke/mume wake umtukane muambia hapana mimi siwezi kufanya hivyo, akimpiga mbele yako acha kuchekelea muambie huwezi kuwa na mwanaume/mwanamke mpigaji, akimdhihaki na kumtukana basi kasirika. Anatakiwa kufahamu kuwa hayo si mambo utakayoyavumilia.

Ukifurahia mwenzako akifanyiwa jua na wewe hupo salama kwani anafanya si kwasababu ya ushetani wa yule mwingine bali kwasabbau ya ushetani wake. Siku wakiachana hatakua na amani mpaka adhalilishe mtu mwingine na kama uko naye basi utakua ni wewe, kumbuka hata huyo anayemdhalilisha leo hakuanza kwa kumdhalilisha bali kuna wakati walikua vizuri kama mlivyo sasa.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA