Msikilize, Muongoze Aongee amalize,usimpige,;


May be an image of 1 person
4
Hiki ndicho kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kumfanyia mwanamke, msikilize, muache aongee, muache alalamike na muache ashutumu hata kama anakushutumu wewe.
Katika kipindi hiki hakikisha unamuunga mkono na mfanye ajione yuko sahihi hata kama hayuko sahihi. Akiwa na mawazo si wakati wa kumsuta, kumshutumu au kumuumbua, hapana ni wakati wa kumsikiliza na kuwa pale kwaajili yake.
Kwamba hata kama amefanya kosa yeye lakini hembu muelewe, onyesha kua unaelewa upande wake kwanini amefanya lile kosa na utalirekebisha baadaye. Kwamba baadaye akishatulia ndiyo utamuambia lakini hiki ungefanya hivi na kile kingekua vile.
Pia inawezekana si muongeaji, niwale watu wa kuficha vitu, hembu msaidie ili aongee, ili afunguke na kuondoa sumu mwilini. Kwamba akisema kua sina tatizo usikubali kubali tu, mkumbatie, mdekeze ili akuamini.
Akishakuamini atafunguka na kuongea kila kitu kinachomkwaza, mara nyingi wanawake huamua kubaki na mambo kwakua tu wanaogopa kuongea au wanaona hata wakiongea hawatapata msaada wowote.
Kwamba kama kila mara akiongea unamkatisha, unamsuta na kumdharau, humsikilizi unaonyesha kutokujali na kuona kama anaongea ujinga basi hataongea kabisa, kuwa msaada wake ili awe huru kuongea na kutoa sumu mwilini.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA