NILIMUACHA MKE WANGU KWAKUA HAZAI ILA SASA NALEA WATOTO WA MWANAUME MWINGINE!



Mada yako imenigusa sana, miaka saba iliyopita nilikua katika hali hiyo. Nilikaa kwenye ndoa kwa miaka miwili na nilikua nataka mtoto sana. Mimi ndiyo wa kwanza kwetu hivyo ndugu zangu walikua wakiongea sana.

Niliona kama mke wangu hazai, nilimtafuta X wangu na kuongea naye kuhusu ishu ya mtoto, nikaomba kurudiana naye, mimi nayeye, hatkua na mtoto kabla lakini niliona kama mke wangu ndiyo ana matatizo.

Nilipomuambia X wangu kuhusu kurudiana naye hakubisha, nilirudiana naye na haukupita mwezi akabeba mimba yangu. hapo ndipo niliona raha ya maisha, nilimpeleka kwetu na kumtambulisha, Mama yangu alimpenda, ndugu zangu wakawa wananiambia nimuache mke wangu.

Kwakua nilikua nampenda mke wangu na kusema kweli tulifanya mambo mengi pamoja ilikua ngumu kwangu, ila Mama alimletea yule mwanamke mpaka wkangu wakati akajifungua, yaani katika nyumba amabyo nilijenga na mke wangu tena yeye ndiyoa lichukua mkopo.

Nikajikuta namchuklia mke wangu, akiongea kitu namuambia ondoka basi ikawa shida, hakuondoka lakini Baba yake aliposikia alikuja na kumchukua binti yake na kulazimishia talaka. Mke wangu hakudai kitu chochote, aliondoka na kuendelea na maisha yake.

Nilipata mtoto wa kwanza na hatimaye wapili, nyumba ilikua na amani kidogo, ingawa nilikua simpendi sana lakini nilimvumilai X wangu kwasababu ya watoto na ndugu. Mwaka jana miaka sita baadaye mtoto alikua akichezea simu ya Mama yake.

Basi katika kuangalia niliona meseji imeingia, ilikua ni meseji ya Whatsapp, basi nilishangaa kwani Whatsapp ya mke wangu naijua na niko huru na simu yake, lakini kumbe anazo mbili kwenye simu hiyo hiyo moja anatumia ile Parallel.

Nikajikuta naingia na kusoma, alikua akichart na mwanaume ambaye anaonekana alikua ni X wake na ni mume wa mtu. Alikua anamuambia kuwa anataka mtoto wa tatu kwakua anataka kumaliza kuzaa na kutulia na mume wake. Yaani ukifuatilia mazungumzo yao unajua kabisa kuwa watoto wote watatu si wangu.

Alikua na huyo mwanaume mume wa mtu tangu kipindi niko naye kwenye mahusiano yaani ile mara ya kwanza, huyo mwanaume ndiyo alimsomesha chuo, alikua anamsaidia kila kitu, yaani kipindi niko naye chuo namuita mpenzi wangu alikua naye, kumbe yeye ndiyo alimuambia tuachane ndiyo maana alinifanyia vituko lakini wakaja kugombana ndiyo maana nilipomuambia kuhusu mtoto hakubisha.

Alibeba mimba ya huyo jamaa baada ya kumuambia kuwa nataka sana mtoto na kumbe yeye tangu mwanzo alikua anahisi nina matatizo kwani nimeona mesejiz ake nyingi akilalamika mbegu zangu ni nyepesi sana. Watoto wote kazaa na huyo Baba na ni mara nyingi sana anawapeleka kuwaona watoto wake na anawahudumia.

Hata shule anayosoma mtoto wetu wa kwanza ni yeye hulipia nusu kwakua mimi na mke wangu tulikubaliana kuchangia kwani ada ni kubwa, namuona anafanya kazi najua anatoa pesa kumbe ni mwanaume mwingine. Nilipoma na kuambiwa kuwa mbegu zangu ni nyepesi sana siwezi pata mtoto nikahangaika hospitalini kuna dawa nilipewa na kweli nilianza kuona kama mbegu zangu zinakua nzito.

Sikumuambia mke wangu kitu chochote, sikumuambia kama nimeona, nilihisi kuchanganyikiwa, kilikua ni kipindi kigumu sana kwangu kwenye maisha yangu. Nilihangaiaka sana na mazoezi, niliacha pombe na kutumia dawa vizuri ndipo nilifanikiwa kupata mtoto na mke wangu.

Sasa hivi nina watoto watatu, wawili ni wa huyo mchepuko wake na mmoja ni wakwangu. Mke wangu hajui kama ninajua ila kwa kuwanagalia wanangu tu huyu mdogo ni tofauti kabisa. Mke wangu wa zamani ameolewa na ana watoto wawili, najaribu kujipa amani kuwapenda hawa watoto wengine lakini bado moyo mgumu, bado naumia na najutia mwanzo kwanini sikwenda hospitalini kuchekiwa kwa kuamini wanawake tu ndiyo wanakua na matatizo.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA