HUYU UNEYEMUITA RAFIKI YAKO NI MNARFIKI KULIKO HUYO ANAYEKUTANGAZA!




Ukiona mtu anajiira rafiki yako, halafu kila siku anakueltea umbea namna unavyosemwa huko mtaani. Yaani kila siku akija ni falni kasema hivi flani kasema vile, narudia yaani yey kila akija kwako anakuambia jinsi unavyosemwa huko nnje.

Unalia anakubembeleza na kujifanya kukupa ushauri ila hakomi kukuletea umbea basi jua mambo hayo.

(1) Huyo mtu ni mshenzi, shetani nmnafiki na mzandiki uliko hao wanaokusea, yaani anakuletea umbea ili uumie, anatamani maisha yako, anahani una furaha hivyo anakueletea vitu vya kukuchoma.

(2) Asilimia 90 ya umbea ni uongo, mengi anayokuambia ni yale ambayo yanamchoma. Kwa mfano, anakuambia kuwa “Flani anasema unaringa na mume wako lakini mume wako ni malaya!” basi huyo ni kama alikua anataka kukuambia muda mrefu kuwa unaringa ila hakupata nafasi ni yeye anataka kukutukana si hao anaowasema.

(3) Kuna kitu anakuonea wivu na ni muda mrefu anataka kukushusha, ana maisha mabovu hivyo anaumia na anataka nawe uumie.

(4) Rafiki wa kweli anakionya kuhusu mtu flani, kwa mfano, atakuambia, Annaeee kuwa makini na flani maana mambo anayoongea mtaani sio, baada ya hapo ataachana na huyo flani na hatakueletea umbea tena mpaka asikia kitu cha kukudhuru labda wanataka kukupiga au kukuua.

(5) Adui yako hawezi kukusema mbele ya rafiki yako. Mtu ambaye ni rafiki yako hawezi hawezi kukaa kusikiliza umbea kila siku unasemwa, atawaona hao watu hawafai atakaa nao mbali. Ila kama kila siku wanakua naye, wanakua huru kuongea basi huyo si rafiki yako ni mnafiki mwenzao.

CHA KUFANYA NI NINI? Mara ya kwanza muambie kabisa kuwa, sikiliza, ukisikia umbea kuhusu mimi huko mtaani kaa nao, sitaki kabisa kuusikiliza ina furaha zangu hivyo sitaki.

Basi akigoma, siku anakuja kukuambia flani kasema hivi, mkatishe kisha muambie “Ndugu yangu, hayanihusu hayakuhusu, kama kasema mdomo wake, haunihusu!” nyamaza kisha aondoka kabisa asikuzoee.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA