UNAPOOLEWA HAIMAANISHI PESA ZAKE ZOTE ZIISHIE KWAKO!






Kuna wakati unaweza kumuona mume wako ni mzembe, hafanyi mambo ya maendeleo lakini ukweli nikuwa wanaume wana majukumu mengi. Mwanamke akiiolewa anataka kuwa yeye tu kwamba mume aache kusaidia ndugu, marafiki na watu wengine, hivyo akisikia labda mume anapata milioni moja, basi anaipigia mahesabu hiyo milioni moja yote mpaka iishe.

Kama ikitokea kwamba haoni matumizi yake hapo nyumbani basi huihsia kulalamika. Dada zangu kuna ndugu zake, kuna kuweka akiba na wakati mwingine pia kuna marafiki wa kusaidia. Kuna watu wengine walimsaidia huko nyuma mpaka kufanikiwa ambao anapaswa kuwasaidia hivyo kabla ya kulalamika kuwa pesa yake huioni hembu fikiria ana majukumu gani?

Kama una mwanaume ambaye analeta chalula nyumbani, anahakikisha analipa kodi hamlali nnje hambu punguza kasi ya kulalamika. Acha kumlianganisha na mume wa shoga yako au dada yako ambaye anafanya kazi kama yake kwani hujui majukumu yake, hawezi kuacha kusaidia ndugu zake kwakau tu kaoa. Inawezekana unaongea kwakua ndugu zako hawahitaji msaada kwako ila wangekua wanauhitaji usingewaacha kuteseka!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA