KUA MAKINI NA MWANAMKE WA NAMNA HII NI KASHETANI KADOGO!






Kuna yule Mwanamke ambaye ni mtu mzima kidogo kuliko mume wako. Anaweza kuwa kaolewa, hajawahi kuolewa kabisa au aliolewa ndoa imemshinda. Lakini yuko karibu na mwanaume wako na amekua karibu na wewe pia, anakuchukulia kama mdogo wake na mara nyingi anapenda kukushauri kuhusu Ndoa yako au mahusiano yako.

Kila mkigombana ukimpigia yeye unakuta mwanaume anaingia laini, anamsikiliza yeye kuliko mtu mwingine yoyote yule. Lakini haishii hapo, ni kama anataka kuwapangia maisha yenu, anataka kila kitu kipitie kwake, mwanaume akitaka kufanya kitu cha maendeleo atataka kushiriki, kuchangia mawazo na kuwashauri.

Mfano mnataka kununua kiwanja, atataka kushiriki kujua mnanunua wapi, namna ya kuandika majina au hata kumuambia mwanaume asinunue kiwanja. Anamsikiliza mwanaume wako kiasi kwmaba mkigombana au msipoongea kidogo tu mwanaume anakasiruika, anataka mpatane na kutaka muongee, anakua hana amani kama umemuudhi huyo dada.

Wadada wengi wa namna hii ni wapweke, wengi unakuta ndoa zao zina shida au walishaachika au hata ndoa hawajawhai kuisikia lakini wanajifanya ndiyo wanasjililia ndoa yako. Kwa mwanaume anamuona huyu mwanamke kama Mama, anamuamini kwakua ni mkubwa kidogo na anamuelewa, kila saa akiongea kitu basi wmanaume anaona ndiyo sawa.

Hawa wadada wanajifanya kusaidia lakini hakuna watu washenzi kwenye ndoa za watu kama hawa. Narudia, wanajifanya kusiadia ila ni wengi wao ni washenzi, wapo baadhi ni Dada wakubwa kweli ila ukiona anazidisha na kuanza kuwapangia mambo ya ndani basi jua huyo ni wale washenzi.

Yaani hao ndiyo huamua mume anaune, sijui aongee na wewe, akupe pesa na vitu kama hivyo. Kama mume wako ana mtu wa namna hiyo, Mama wa hiari basi usimnunie lakini usimuweke karibu,a cha kumuambia matatizo ya ndoa yako, yaani ni bora kwenda kulilai chooni kuliko kuwaambia watu hawa.

Ukweli nikuwa, ukimuambia atajifanya kukusaidia, kwakua anamcontrol mume wako basi atamuambia ongea na flani, ila atampa masharti, atafanya vituko mpaka utachanganyikiwa. Hamtakuja kuwa na amani, anaweza kumuambia mume wako asikupe hela ili uende kulalamika kwake na ukishalalamima anamuambia akupe ili tu umuone kama Mungu!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA