KAMA UNASAMEHE ACHA KUWAKA MASHARITI




Moja ya kitu ambacho kinachanganya wanawake wengi ni pale waume zao wanapochepuka na kuzaa nnje ya ndoa. Wanawake wengi wanasamehe waume zao, ni wanawake wachache sana ambao mwanaume anazaa nnje ya ndoa na kumuacha mwanaume kwakua kazaa nnje ya ndoa. Hili si tatizo lakini tatizo linakuja pale ambapo wanawake wanaposamehe lakini kwa mashariti.

Iko hivi, unapomsamehe mume wao mchepukaji basi jua kuwa huna tena haki ya kumpangia namna ya kumlea mtoto wake. Wengine utasikia anakuambia “Sawa lakini huyo mtoto sitaki kumuona hapa kwangu… sitaki uwe unamtumia pesa… sitaki uwe unaenda kumsalimia… sitaki upost picha zake… sitaki hiki, sitaki kile sitaki kile”

Dada yangu achana na hayo mambo ya sitaki, ni kweli unaweza kusema nakusamehe lakini mimi siwezi kumlea mtoto wako, abaki na Mama yake, ni jambo zuri pia kwa mtoto kubaki na Mama yake, lakini kama mwanaume akiangalia na akaona kuwa mtoto wake kuwa kwa Mama yake hatakua salama basi huna tena maamuzi ya kusema siwezi kumlea.

Na hapa nataka muelewe, mwanaume anapomchukua mtoto wake na kumlea si kwamba anakuchukua kuleta umlee, hapana, kama Baba anabeba majukumu yake ya kulea mwanae, lakini kinachotokea nikuwa kwakua wewe unaishi naye basi inabidi msaidiane kulea. Labda niwaulize dada zangu, mfano wewe una mtoto, unakutana na mwanaume anataka kukuoa ambaye si Baba wa mtoto.

Lakini anakuambia kuwa nakuoa ila mtoto muache kwa Baba yake, sitaki kumuona kabisa, sitaki umpost mtoto wako kabisa, sitaki mtoto wako umfanyie hivi na vile! Je, utachagua mwanaume au mtoto? Mwanamke yoyote mwenye akili atachagua mtoto na kumuacha huyo mwanaume, kwa maana hiyo basi hivyo hivyo mwanaume. Ingawa ni vizuri mtoto kulelewa na Mama yake lakini kama kuna ulazima wa kumchukua na mke wako hataki basi muambie Mama njia nyeupe.

Hakuna haja ya kusumbuana! Kuna mazingira mwanamke anaweza kukataa, labda mwanaume anaenda kuza atu huko nnje analeta mwanamke alee, hapo no! Labda huyo Mama wa mtoto ni kila siku anapiga simu kutukana hapo no! wakati mwingine mwanaume ana watoto kibao lakini hahudumii, hapo no! ila kikawaida basi ukisamehe jua huwezi kumpangia namna ya kulea!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA