TOFAUTI KATI YA WANAUME NA WANAWAKE AMBAYO WANAWAKE WENGI HAWAIJUI!
Unapomkosea mwanamke ukawa unamuomba msamaha, anakuambia sitaki, sikutaki, ondoka, akakublock na kutotaka kabisa umtafute basi jua kuwa anahitaji umtafute.
Kakublock lakini anataka utafute namba nyingine ili ujaribu kuongea naye, anahitaji utafute rafiki zake, ufanye kila namna ili kumuomba msamaha. Kama ukikaa kimya kwakua kakublock basi mwanamke huumia na ndiyo unaharibu kabisa.
Lakini sasa kama umemkosea mwanaume, akakuambia anahitaji muda, akakuambia usimtafute, akakublock, akawa hataki kujibu meseji zako na hataki chochote kuhusu wewe. Ukilogwa ukazidi kumtafuta, ukatafuta na namba nyingine, ukatafuta marafiki zake na kuwaambia matatizo yenu, ukatafuta na ndugu zake ili waongee naye.
Ukatuma meseji milioni kuomba msamaha basi jua kuwa ndiyo unaharibu, ndiyo unamuonyesha kuwa huna thamani na huyo mwanaume atakuacha kabisa. Unapomkosea mwanaume fanya juhudi za kumuomba msamaha, mtafute yeye kama yeye, akikuambia umpe muda basi mpe muda kweli.
Acha kuhangaika kwa ndugu zake, marafiki na watu wengine. Mpe muda labda wa wiki moja, sasa angalia kama atakutafuta au la, ukishampa muda kidogo kichwa chake kikatilia basi mtafute, mtumie hata meseji lakini si za kuomba msamaha tena bali mikumbuke.
Fanya juhudi za kumtafuta wewe kama wewe, kujaribu kuwasiliana naye na kujulia hali kwa meseji ambazo si za kulalamika sana au kuomba msamaha kila saa. Akizidi kukuambia umpe mdua hataki kukusikia kaa kimya tena kwa muda hata wa wiki, mpe nafasi kama anakupenda atarudi kama alishakuchoka basi jua kuwa ndiyo mwisho ila kulazimishia kusamehewa hakuleti msamaha.