MWANAUME WANANIAMBIA NIWE MAKIINI NISIBEBE MIMBA JE ANANIPENDA?
Kaka vipi mwanaume akikuambia kuwa makini na siku zako usije beba mimba anamaanisha nini?
JIBU LANGU; Kwa wanawake wengi ukimuambia hivi wanadhani kuwa hawapendwi, wanajisikia vibaya na kutaka kuachana na mwanaume husika. Hii ndiyo sababu wanawake wengi wakitaka kumpima mwanaume kama anampenda au la huanza kwa kumuambia nina mimba yako.
Mwanaume kama akipaniki basi wanahdani hawapendwi, ila mwanaume akikubali mimba basi wanaona kama ndiyo upendp. Ukweli nikuwa, hiki ni kipimo cha hovyo kabisa, mwanaume anaweza kukubali mimba, akakuambia mzae lakini bado akakuacha.
Kama unanisoma sana nilishasema wanaume wengi hukataa mimba zikishafikisha miezi mitrano mpaka sita au mtoto akizaliwa. Hivyo kumuambia mwanaume nina mimba yako akakuambia zaa tutalea haimaanishi kama anakupenda, wala haimaanishi kama atakuoa, au hata kama atahudumia mtoto hapana, inamaanisha kuwa kakubali ili usitoe mimba.
Sasa swali lako je mwanaume anaweza kuwa anakupenda lakini aakakuambia usibebe mimba yake? Ndiyo, na kwa mimi mwanaume anayekupenda sana atakuambia mambo ya mimba hapana. Hii ni kwakua mwanaume anajua kabisa kuwa kua mahusiano na mwanamke si lazima ndoa, kuna mambo yanaweza kutokea katikati.
Anakuambia kuwa makini ili usiharibu maisha yako, anakuambia kuwa makini kwani hajawa tauari kuoa, anakuambia kuwa makini kwakua anajua ukibeba mimba yake utaanza kulalamika sana na hata kuishia kugombana na kuachana. Kwa maana hiyo, kuwa makini kweli na kama ni suala la ndoa litakuja muda ukiwa tayari na kama ni kuachana hata hao wanaosema zaa nitakuoa nao wanaachana.