BIASHARA YAKO INAKUFA KWAKUA WEWE MWENYEWE UMEITELEKEZA!


Rafiki yangu mmoja amefungua Duka la nguo, bado changa na hana wateja wengi. kwakua ni mfanyakazi basi muda mwingi anakua kazini, ameajiri mtu. Sasa nilshamshauri, kuwa kama umefungua Biashara hakuikisha kila muda wa ziada unaoupata unakua dukani kwako.
Watu uliowaajiri wapo tu na wanaondoka siku yoyote, wewe kama mmiliki unapaswa kutemngeneza wateja wako. Kuna namna ambavyo mmiliki anaongea na wateja, anakaribisha kwakua ana uchungu na mtaji wake kuliko mtu uliyemuajiri. Nikamuambia kuna watu watakuja kununua kwakua wanakujua na si kwakua una nguo nzuri.
Niliongea naye sana na alionekana kunielewa, lakini mimi nikajipoa kazi ya kupita dukani kwake kila baada ya muda wa kazi na siku za weekend. Nakuta tu msichana wake yeye hayupo, siku moja nikamuuliza mbona huonekani dukani. Kaanijibu “Hakuna wateja, panachosha hata kukaa…”
Nilimuambia funga tu duka ondoka Biashara haikufai. Akaniuliza, kwanini nikamuambia, kama wewe unachoka kukaa dukani kwako ni nani atapapenda, umepakatia tamaa, huyo uliyemuajiri sinaye atapakatia tamaa, ataanza kuiba kwakua anaona hakuna kitu, wateja watapakatia tamaa, kaa dukani kwako hata kama huuzi lakini ni kwako.
Duka ni kama mtoto, humkatii tamaa mwanao kwasababu yoyote ile, ukimkatia tamaa mwanao jua hata majirani hawatamjali. Kaa dukani kwako, jua Biashara yakompaka pale itakapoanza kutengeneza gaida, najua unasoma hapa, kinachoua Biashara yako ni kwakua hukai dukani kwako, umeikatia tamaa unafikiri uliyemuajiri atafanyaje?
May be an image of 2 people and indoor
Like
Comment
Share

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA