MWANAMKE! TAMBUA KUWA MWANAUME MWENYE NIA YA KUKUOA HUWA HANA KISINGIZIO CHA KUSEMA ANAJIPANGA
Mwanaume anayetaka kukuoa kwa na kweli anakupenda hawezi kuacha kukuoa kwa sababu ya kutaka kujipanga, maana atahofia asipokuoa atakupoteza, utaolewa na mwingine,
Anayekupenda, atakuoa, japo anaweza tu akasema nakuoa ila hatutazaa kwanza wakati tunajipanga ki maisha, ila kukuoa atakuoa maana wewe ndio furaha yake, wewe ndio mshauri wake na wewe ndio anakuona mhimu kwakwe, ila ukikutana na mwanaume anasema atakuoa ila siyo muda sahihi sasa,huku bado anafanya vitu vya maendeleo peke yake jua tu hapo UNAPOTEZA WAKATI,
Kama ni maendeleo na wewe anakuona ni mama wa familia yake, ataona ndio wakati wa kuja kufanya hayo maendeleo akiwa na wewe
Ataona ni mhimu wewe kushiriki maendeleo hayo kwajili ya familia na watoto huyo ndio anakupenda..
Ila ukiona unaambiwa nitakuoa ila siyo muda mwafaka sasa jua, una sifa zote za kua mke bora ila kuna vitu hajapendezwa na wewe, inawezekana siyo mzuri sana wa sura kama mwanamke anayewaza kumwoa, au kuna vitu unakosa chumbani alisha wahi kuvipata akavipenda akaweka kua ni moja ya sifa ya mwanamke wake wa ndoa ila sasa wewe huna..
Anapata ugumu wa kukuoa huku anajua akikuoa ndio mpaka mwisho wa uhai..
Hapo ndio anakuambia kauli hiyo kua atakuoa ila usubirie muda ukifika atafanya hivyo.. Ili wakati una msubilia aendelee, kutafuta wa sifa anazozitaka, akimpata hata kesho yake tu utasikia kamtambulisha mtu na kaoa..
Na ukiwakuta wanaume wa hivi akikosa hilo chaguo lake na akamua kukuoa tu, wana kuaga ni watu wa michepuko sana
Ili kuendelea kukitafuta nje kitu ulichokosa wewe na akikipata anaweza hata vunja ndoa akaenda kuishi na huyo aliyempata.. Au hata akawa msaliti sugu tu yaani akawa anatoka nje ya ndoa wazi wazi na mchepuko wake ukajua kabisa..
Maswali ya kujiuliza kama anataka kunioa badae lakini bado anafanya maisha ya maendeleo peke yake ananioa mimi ili nikawe nani sasa?
Kama mke ni msaidizi wa mwanaume lakini yeye sasa anafanya kila kitu peke yake na anadai atanioa anataka nikamsaidie nini?
Kama anachokifanya ni kwaajili ya familia yangu na yeye kwa nini haoni umhimu wa kuoana ili na mimi nikashiliki?
Haya maswali ya nakupa picha kwamba anachokitafuta wewe hakikuhusu, maana hana lengo lolote na wewe
Huwezi kunielewa leo🖐️