KARIBU KATIKA SOMO LETU. ✍️✍️
*----•<°○●πππ●○°>•----*
ππUzuri wa mwanamke unapatikana kwenye ulimi wake.Tuache tabia ya jeuri na maneno machafu,kiburi na dharau hakika tabia hizi zinamchukiza kila mwenye akili.
*ππKAZI KWANZA*
Baadhi yetu tunathamini na kujali kazi zetu na hatuna muda na mahusiano yetu.
*ππWATOTO KWANZA MUME BAADAE* (KWA WANANDOA)
Kuna baadhi yetu tukishakupata watoto mapenzi yote yanaelekea kwa watoto na tunamsahau baba watoto.
*ππKUTOKUA NA SHUKRANI*
Hii ni tabia sana itayomchokesha mumeo na aondoshe mapenzi kwako, kua na shukrani kwa yale anakufanyia ndipo atakapopata moyo wa kukufanyia makubwa zaidi.
*ππKUTOKUA MUELEWA*
Kuna baadhi yetu tunakua ving'ang'anizi na tukitaka kufanya letu hata tukakatazwa hatuskii wala hatujali kua tumeolewa tuwe wenye kutii waume zetu.
*ππUSIRI*
Tuko baadhi yetu tunakua tunawaficha waume zetu kila kitu hatuwafanyi wao kua ndio washauri wetu.
*ππKUKOSOA KILA JAMBO*
Tuache tabia ya kukosoa na kugombana Kwa kila jambo ,hata akikosea mueleweshe Kwa njia za kistaarabu.
*ππKUTAKA WEWE UWE BOSS*
Mungu aliyetukuka amewapa cheo wawe viongozi wetu na wasimamizi kwetu hatuna budi kulikubali hilo,acha kujifanya wewe ndio Kichwa cha nyumba lazima umheshimu na ajue kua anaheshimiwa .
#KUMBUKAππ Hekima yako inaweza kubadilisha tabia mbaya MPENZI wako kwa asilimia kubwa.Pia ujeuri sio dili jamani tubadilike katika hili.ππ

