π1.KILA UNAEMUOA AU KUOLEWA NAYE ANA UDHAIFU WAKE.*
*
Mungu
pekee ndio hana udhaifu,
Kila ua waridi lina chimbuko lake.
*
2.KILA UNAEMUOA AU KUOLEWA NAYE ANA HISTORIA YAKE MBAYA.*

Hakuna mtu ambaye ni malaika,
epuka kuchunguza mambo ya mtu ya nyuma samehe na usahau.
*
3.KILA NDOA INA CHANGAMOTO ZAKE*

Ndoa sio kitanda cha maua waridi yanayomeremeta kila muda,
kila ndoa yenye mafanikio imepitia misukosuko mingi.
*
4.KILA NDOA INA HATUA ZAKE KATIKA MAFANIKIO*

Hatuwezi kuwa sawa,
kuna watakaokuwa mbele kidogo na watakaokuwa nyuma kidogo. Kupunguza stress, kuwa mtulivu, fanya kazi kwa bidii na kwa muda muafaka ndoto za ndoa yako zitatimia.
*
5.KUOA AU KUOLEWA NI KUTANGAZA VITA*

Ukishaoa au kuolewa ni kuingia katika uwanja wa mapambano,
Kuwa tayari kupambana kuulinda ukanda wa ndoa yako.
*
6.HAKUNA NDOA ILIYOKAMILIKA.*

Hakuna ndoa ambayo imetimilika,
Ndoa ni kazi ngumu,
jitolee mwenyewe na ufanye kazi ya kuijenga ndoa yako iwe kamilifu.
*
7.MUNGU HAWEZI KUKUPA MTU KAMILI UNAYEMTAKA.*

Mungu atakupa mtu ili wewe umtengeneze jinsi wewe unavyohitaji yeye awe.
*
8.KUOA /KUOLEWA NI KUJIINGIZA KATIKA HATARI.*

Huwezi jua nini kitatokea baada ya ndoa,
hali inaweza badilika,
hivyo achia nafasi ya marekebisho.
*
9.NDOA SIYO MKATABA WA MUDA BALI NI MKATABA WA KUDUMU.*

Ndoa inahitaji ahadi ya kudumu,
mapenzi ni gundi ambayo huwafanya wanandoa kuwa pamoja daima..
Talaka huanza katika mawazo.
*
10.KILA NDOA HUHITAJI KUJITOA.*

Hakuna mapenzi rahisi katika ndoa,
huwezi kupenda au kupendwa bila kujitoa nafsi yako kwa dhati...
Share