HII NI MIONGONI MWA KAULI ZA KIJINGA NA KIPEPO KUSEMA KUWA MWANAMKE HANA DINI

*

Huu ni moja ya msemo wa wanadamu unaotumika hasa kwa mwanamke anapotakiwa kuolewa na mtu wa imani tofauti na yeye.
Wanaposema mwanamke hana dini wanakuwa wanamaanisha kwamba mwanamke hana haki au uhuru wa kuwa na msimamo wake binafsi wa kiimani.
Basi watu huwa wanamshauri binti wakisema,
wewe olewa tu bwana mwanamke hana dini yeye popote tu anaenda.
Wakiwa wanamaanisha kwamba kile anachokiamini mume atakayemuoa ndicho atakachokiamini na yeye.
Yaani kama yeye anamuamini au anamuabudu Mungu aliye hai na anayetaka kumuoa anaabudu mti,
basi aachane na Mungu aliye hai afuatane na mume wake waanze kuabudu mti.
Mwanamke,
huu msemo si kweli kwamba wewe hupaswi kuwa na msimamo wako wa kiimani au wa kuabudu.
Wanawake na wanaume sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu,
siyo kwamba watakaohukumiwa ni wanaume peke yao.
Ukiruhusu ndoa ikakutoa kwenye imani yako na kukupeleka kwingine hiyo ni juu yako,
Mume wako,
ndoa yako wala watu waliokushauri olewa tu hawatakusaidia usiende Jehanum.
Binti usiwe mjinga ndoa haijakusudiwa ikutoe kwa Yesu,
wala katika kumtumikia Mungu,
Na wala Mungu hajaiweka ndoa ili imzuie mtu kwenda mbinguni.
Bali imekusudiwa kukufanya bora zaidi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Follow my page
Share
May be an image of child, standing, twilight and sky


DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA