JE UMESHAWAHI KUCHEPUKA BILA SEX
Najua watu wengi wanajiuliza unawezaje kuchepuka bila ya kukutana kimwili.
Ila hiki kitu kipo sana na huenda tunakiona cha kawaida na kinaweza kukuharibia ndoa yako au mahusiano yako.
*Utajuaje kama unachepuka bila kusex,?*
twende pamoja tujifunze.
Je kuna mtu tofauti na mwenza wako unamfanyia yafuatayo?

Je kuna mtu wa jinsi tofauti na wewe unavutika kuwasiliana naye zaidi kuliko mwenza wako,
hata kama unamchukulia kama rafiki wa kawaida ila ujue huyo ni sawa sawa na mchepuko kwako.

Kuna yule mtu ambaye si ndugu yako lakini huwezi kumaliza siku bila kuwasiliana naye.
Unaweza ukasema anakufariji au anakuchekesha ila jua unachepuka kifikra.

Ni rahisi kumueleza siri zako kuliko unavyomueleza mume au mke wako,
jua huyo ni mchepuko wako wa kihisia.

Mwanzo huenda ulikuwa unamuambia mwenza wako kila mtakapowasiliana ila baadaye hutaki ujulikane kama unawasiliana naye zaidi,
basi jua unachepuka kihisia.

nakuta una rafiki wa jinsia tofauti na unapenda kutoka naye Sana kuliko mwenza wako na huenda hajawahi kukutongoza wala hamjawahi kusex,
ila unapenda kuwa karibu naye zaidi.
Basi jua huo ni mchepuko wako wa kihisia.
Usipojizuia mapema Unawezajikuta unampenda na kuharibu ndoa au mahusiano yako.
Hivyo kila kitu kwenye maisha yako kiwe na mipaka.
Follow my page
Share