Kama wewe ni Mchepuko ni Mchepuko tu acha kucheza nafasi ya mkewe kua na Maisha yako
Utasikia anasema, anampenda mke wake lakini hata mimi ananiheshimu, ananipenda, sio kama ile michepuko yake mingine. Mimi ana ni treat vizuri. Ndiyo unajiambia hivyo huku ukiwaangalia wale ma Bar maid, ukiwaangalia wale wanafunzi na wale wake za watu wengine ambao anatembea nao.
Umejipa kakazi flani ka mke, kwavile unadhani kuwa wewe nawe una kathamani. Eti unajiona kama ni “Ka Lady” fulani basi wewe humchuni sana na unakuwa mtu wake wa kumsikiliza, kusikiliza matatizo yake na mkewe, kusikiliza matatizo ya kazini kwake.
Lakini ulivyo hujithsmini, hata akiwa na shida anakuja kwako, ndiyo anakuja kukukopa na wewe unajiambia kuwa anakupenda, sina uhakika kama unawaza kuwa atakuja kumuacha mkewe labda na kukufuata wewe au unaona sijui ipo siku atakuja kuachana na michepuko mingine na kubaki na wewe tu!
Yaani unaharibu na dua zako kabisa kwa Mungu kuomba aachane na michepuko mingine ili uwe mchepuko wa pekee! Dada yangu si heri tu hata ungeomba makontena ya makinikia yadondokee kwenu au uombe uokote vichwa vya treni!
Dada yangu kama u mchepuko u mchepuko tu! Hembu acha ku act as a lady, acha kujifanya wife material, unajifanya kumshauri sijui ajenge, sijui afanye mambo ya maana! Chukua nafasi yako kama mchepuko, mechi urudi kwako ndani ukalale peke yako ukiangalia paaa tu, huku ukimuomba Mungu akuletee mshamba mshamba wa kukuoa!
Wewe ni mchepuko acha kufanya kazi ya mke, acha kujipa moyo kua una tofauti na wale wengine ambao anawachezea, wote mko daraja moja hivyo kama ni kuchuna chuna uondoke na acha kumkufuru Mungu! Amka dada yangu mwisho wa siku atarudi kwa mkewe na kukutumia kama ushuhuda!
Wakati akisema kuwa mke wangu nisamehe ni shetani alinipitia atakuwa akimaanisha wewe! Wakati akisema kuwa niliteleza atakuwa akimaanisha wewe! Hapo tayari atakuwa ashakuzalisha huna soko tena, hakutaki au mkewe kashamuambia kama unataka tuendelee basi achana na yule Malaya! “Anamaanisha wewe ndiyo yule Malaya!” Badilika!