KANUNI 6 MUHIMU KWA AJILI YA MAHUSIANO YAKO

 

*👉1:MFAHAMU VIZURI MTU UNAYEHUSIANA NAYE;*
Awe ni mke au mme wako, hakikisha unamfahamu vizuri
Na kama hamjaoana,
muda wa mahusiano hadi uchumba ndio
muda mzuri
wa kufahamiana kuelekea kwenye ndoa.
Hakikisha unamfahamu katika maeneo yake tofauti tofauti,
Je Yeye ni mtu wa aina gani
(haiba gani) ?
Anapenda nini ?
Kitu gani hapendi ?
Hali yake ya mahusiano na Mungu ikoje ?
Je uchumi wake uko vipi ?
Je marafiki zake ni wapi ?
Je unazifahamu ndoto zake za maisha ?
Je anapenda miziki gani ?
Je ndugu zake wa karibu ni wapi ?
Je anaabudu wapi na nani anamlea ?
Je anapendelea mlo gani sana ?
Je anapenda kusoma kitabu gani haswa ?
Je unazo ndoto zipi hapo mbeleni ? Na je umechukua hatua gani kuwa mtu huyo unayetaka kuwa ?
Je unataka maisha yako yawe vipi baada ya miaka 5 ijayo ?
Ni nani anakuhamisisha na unataka kuwa kama yeye ?
Ukiweza kuyafahamu hayo na mengine mengi itakusaidia uweze kuishi naye Vizuri na kusaidiana vizuri.
Kumfahamu vizuri mwenzi wako husaidia kupunguza migogoro mingi ya kwenye ndoa.
Tenga muda wa kuongea naye ana kwa ana
Tafuta eneo zuri la utulivu wakati mnaendelea kula mnaendelea kuongea na kusemezana mambo mbalimbali juu ya mahusiano yenu na kufahamiana zaidi.
Kadri ambavyo mnafahamiana ndivyo ambavyo mahusiano yenu yatakuwa imara.
*👉2:ENDELEA KULINDA ,*
*KUKUZA NA KUTUNZA UPENDO WAKO KWA MWENZI WAKO KILA SIKU*
Kama utaweza kuendelea kumpenda mwenzi wako na kutunza upendo huo kila siku,
basi maisha yenu ya mahusiano yatakuwa mazuri kila siku.
Kumpenda na kuendelea kumuheshimu mwenzi wako kila siku ni nguzo muhimu sana kwa upendo wa kila siku wa mahusiano,
na itaepusha usaliti mwingi.
Tafuta njia mpya kila siku za kumuonyesha kuwa unampenda ,
Fanya kwa vitendo na muambie pia kwa maneno,
Endelea kutunza heshima kwake kila siku.
Mfanye ajione kuwa unamkubali kila siku kwa kumumbia na kumuonyesha kwa vitendo,
Mshukuru kwa yale anayokufanyia kila siku na kwa yale ambaye hayafanyi mkumbushe umuhimu wake kwa upole na utaratibu mzuri.
Ukimaliza kuongea naye mwambie asante kwa
muda mzuri
aliokupa wa kuongea na yeye,
Kama ni mume wako mwambie asante kwa kuwa mme bora na baba mzuri kwa watoto wangu.
Usitumie maneno makali na hasira kwa mwenzi wako,
Kumbuka anahitaji kupendwa na kuheshimiwa kila siku.
*👉3:ENDELEA KUTAFUTA VITU VYA KUWAFANYA MUWE KARIBU ZAIDI*
Kila muda tafuta kitu ambacho kitaweza kuwaweka pamoja,
Mfano
Kula pamoja,
Kuwasiliana mara kwa mara,
chatting,
normal call na video call
Hakikisha upo in touch.
Mahusiano mengi hufa kwa vitu tu hivyo vidogo vidogo wala sio vitu vikubwa.
Hivyo hakikisha unafanya na kuchagua kutafuta vitu vya kuwaweka karibu zaidi kila siku.
Usiruhusu kitu chochote kishike nafasi ya kuharibu mahusiano yenu,
Ukiwa na mwenzi wako mpe kipaumbele yeye ,
Mfano umeoa umerudi nyumbani hakikisha unampa mke wako muda wa kuwa naye sio unakuwa busy tena na simu au na mambo mengine.
Mke ndio kwanza hata huwezi kumuandalia mme wako chakula uko busy na tamthilia,
Usiendekeze hiyo tabia, hakikisha unampa mwenzi wako muda na unahakikisha upo naye karibu.
Hivyo vitu vidogo vidogo unavyovipuuzia unapokuwa na mwenzi wako ndivyo vinavyojenga mahusiano ya watu wengine unayoyaona yanaendelea vizuri,
Hakikisha unapata muda wa kumuuliza kuhusu siku yake je alikutana na changamoto gani kazini?
Nenda naye kwenye manunuzi, msaidie
Muda mwingine akiwa jikoni unaweza kumsaidia kitu hata kama ni kidogo.
Pata muda wa kusoma naye Neno la Mungu na kuomba naye,
Hakikisha mnapata muda wa kufanya ibada pamoja hapo nyumbani na mnapeana ratiba za kuongoza
Muda wa kwenda ibada toka naye usimuache.
Kama kila mtu ana sehemu yake ya kazi tofauti pata muda wa kumpigia simu,
kuchati naye au ongea naye mpigie video call
Hayo yote ni kutafuta ukaribu.
Jitahidi sana kuwa naye karibu katika hali zake zote za huzuni na furaha, muonyeshe kuwa unamjali katika hali anayopitia
Tambua magumu anayoyapitia.
Kila siku tafuta kitu cha tofauti ambacho kitaendelea kuwaweka karibu zaidi,
*KEEP IN TOUCH*
*👉4:MPE NAFASI YA KUMSIKILIZA NA KUMSHIRIKISHA*
Kanuni ya nne ya kujenga mahusiano yako,
Kuna maamuzi ambayo hupaswi kufanya mwenyewe unapaswa kumshirikisha mwenzako
Na unapaswa kuheshimu mchango wake anaokuambia.
Wanaume wanaowasikiliza wake zao kwenye ndoa imekuwa mchango mkubwa wa mahusiano yenye amani,
Mwanaume anapokuwa na utayari wa kumshirikisha mwenzi wake katika mambo yake ,
ndoa hii huweza kumudu uharibifu.
Na mwanamke anapotii na kuheshimu maagizo anayoyapewa na kupeana na mume wake, ndoa hiyo husimama imara.
Wanaume wengi hawawasikilizi wake zao na hivyo kuleta shida kwenye ndoa,
na hata wanapoambiwa kwanini haunisikilizi hujibu vibaya na kuongeza tatizo badala ya kutatua.
Mfano,
*JIBU LINALOFAA*
Mke: Mbona siku hizi hunisikilizi ?
Mme:Samahani ,
Nakusikiliza sasa unasemaje Mke wangu?
Jibu hilo kidogo huweza kupunguza hasira na mtazamo hasi kwa mke.
*JIBU LISILOFAA*
Mke:Mbona siku hizi unisikilizi ?
Mme:Wengi huweza kupuuzia na kunyamaza au akijibu huweza kujibu ,
Ndio sikusikilizi,
au sikusikilizi sababu hakuna cha maana unaongea au kwanini nipoteze muda wangu?
Kujibu majibu ya hivyo ni ishara kuwa hutaki kumsikiliza wala kumshirikisha mwenzi wako chochote na huleta shida kwenye mahusiano.
Mwanaume ni kichwa cha familia lakini haimaanishi kuwa maamuzi yote anafanya yeye,
Cha msingi ni kujua mipaka tu kwamba jambo hili anapaswa kufanya mke na jambo hili ni mme na mambo haya na haya tunapaswa kuyazungumza mezani.
Kuwa kichwa cha familia haina maaana usimuheshimu mke wako na kumsikiliza
Hapana,
Mme anapompa nafasi mke wake ya kumsikiliza na kumshirikisha katika mambo mbalimbali, hukuza urafiki wao.
*MSIKILIZE NA MSHIRIKISHE ITASAIDIA KUJENGA MAHUSIANO YENU KILA SIKU.*
*👉5:KUWA SEHEMU YA KUTATUA TATIZO*
Mme na mke wanapoheshimiana na kuwa wazi na huru kwa kila mmoja,
basi huweza kuwa na uwanja mkubwa wa kutatua tofauti zao.
Kuna yupo ambaye anaona kabisa tatizo hili linatatulika lakini anatafuta bado sababu za kuendelea kulalamika.
Katika kila tatizo kuwa sehemu ya suluhisho badala ya kumnyoshea mwenzi wako kidole,
Usipende kuwa juu muda wote.
Kuwa sehemu ya tatizo na utoe suluhisho hata muda ambao hukukosea kabisa,
Na katika kila tatizo jaribu kuvaa viatu vya mwennzi wako wakati unaendelea kusikiliza kwa umakini.
Unapokuwa na tatizo na unataka kumueleza mwenzako tafuta namna nzuri ya kumueleza ambayo itafanya maongezi yenu yawe mazuri na yasiyo na shida ,
hata kama umekosewa usianze kwa hasira wala malalamiko mengi bali tafuta namna nzuri zaidi ya kutatua tatizo.
Lalamika lakini usilaumu ,
Lalamika kuhusu jambo lililotekea lakini usimnyoshee kidole yeye kumlaumu.
Kwa mfano, mmekubaliana kabisa kuhusu kitu fulani na unarudi unakuta bado hakijatendewa kazi,
Sema tu kwanini jambo hili halijafanyika na tulikubaliana kuwa litafanyika ,
ingekuwa vyema lingefanyika ingependeza sana.
Badala ya kuanza kusema kuwa
Nilijua tu hutofanya ,
yani wewe ni mzembe kila kitu hufanyi,
Hapana hiyo sio namna nzuri.
Panapokuwa na tatizo pendelea kutumia neno mimi badala ya wewe,
Neno mimi hupunguza maneno mengi kuliko neno wewe.
Mfano,
Wewe hunisikilizi na Mimi naona ungenisikiliza kwanza,
Wewe ni mzembe sana wa pesa na Mimi napenda tutunze pesa nyingi zaidi.
Panapokuwa na tatizo,
Tumia njia ya upole zaidi, mfano Ningependa sana kama ungefanya hivi na hivi pia kutumia neno tafadhali.
*👉6:KUSHINDA VIZUIZI KWENYE MAHUSIANO*
Kila mahusiano kuna tofauti ambazo huwa wanazo lakini wasipotafuta njia ya kutatua hizo tofauti hutengeneza kizuizi kitakachokuwa ni shida kwenye mahusiano yao,
Kila mmoja anakuwa anavutia kwenye upande wake na hakuna mtu hata mmoja anayetaka kujishusha.
Kunakuwepo na mabishano ya kila siku ambayo hayapatiwi suluhisho,
Tatizo linazidi kuongezeka kila siku kadri muda unavyozidi kwenda.
Hizo ni dalili ya kuwa kuna vizuizi kwenye mahusiano yenu,
Jinsi ya kushinda ni vyema kukabiliana na vizuizi mara pale tu unapoona kuna dalili hizo.
Kupuuzia vitu vidogo vidogo kwenye mahusiano imekuwa ni chanzo kikubwa sana cha mahusiano kukwama na kuwa na vizuizi vya kufika mbali zaidi.
Tofauti nyingi kwenye ndoa hutokea sababu ya utofauti wa ndoto 5 hizo huweza kuleta tofauti kwenye ndoa
Kuondoa tofauti hizo wawili wanaohusiana wanapaswa kukaa pamoja na kutatua juu ya hizo tofauti.
Mfano
Mme Yeye anahitaji watoto 4 kwenye familia ,
Lakini mama anahitaji 2
Hii huweza kuleta tofauti na linapaswa kutatuliwa kwa kuhakikisha kanuni ya kwanza tuliyojifunza uwe uliipitia vizuri ya kumjua mwenzi wako vizuri.
Unaweza jiuliza inakuwaje wengine wana ndoto tofauti na bado mambo yanaenda ?
Tofauti iliyopo ni kwamba wenzi wa hivyo hufahamu ndoto za kila mmoja,
na kila mmoja huheshimu ndoto za mwingine na maisha huendelea.
Pia hufanya kazi kama timu na kila mmoja kujali ndoto za mwenzake,
Kushindwa kutambua ndoto za mwenzi wako , shida na vizuizi na tofauti haziepukiki.
Dawa ni kuwa wazi kwa mwenzi wako na kufahamiana kuwa mwenzako anazo ndoto zipi,
Mahusiano ambayo hayaheshimu ndoto ya kila mmoja migogoro haiepukiki.
Kila mmoja anapaswa kuheshimu ndoto na kumsapoti mwenzake kufikia ndoto zake.
Kwanza, Unapaswa kuelewa ndoto za mwenzi wako na kupenda kujua zaidi kuhusu hiyo ndoto
Pili,
Unapaswa kuhakikisha unamsaidia katika hiyo ndoto yake
Tatu,
Kuwa sehemu ya ndoto ,
kufurahi na kusaidiana kutimiza.
May be an image of 2 people, people standing and indoor

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA