MAMA YANGU ALIKUA NI MCHEPUKO WA MUME MCHUMBA WANGU NIFANYEJE?



Habari mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye niko naye kwenye mahusiano mwaka wa tano sasa. Sababu ya mimi kuja kwenu kuomba ushauri ni kuhusu mchumba wangu na Mama yangu mzazi. Mwaka jana ndipo nilimtambulisha nyumbani na kweli walimkubalia na kuanza mchakato, lengo ni kufunga ndoa mwezi wa tisa mwaka huu na kila kitu kimeshakamilika.

Tatizo nikuwa, wiki iliyopita nikikua naangalia simu ya Mama yangu nikakuta meseji za ajabu ajabau alizokua akichat na mchumba wangu. Hazikua za mapenzi moja kwa moja lakini ni kama walikua wanataniana, wanachat kama watu waliokua wanajuana, nilishtuka kiodogo kwani mpaka namtambulisha kwetu sikua najua kama wanafahamiana.

Niliamua kuziacha tu bila kufanya chochote lakini niliamua kuchunguza na siku moja nikafumania picha katika simu ya zamani ya Mama. Alikua ashaacha kuitumia na naamini alidhani kafuta kila kitu lakini niliichukua, ilikua ina tatizo la betri nikaenda kuitengeneza huweza kuamini nilikuta picha za Mama yangu na mchumba wangu wakiwa chumbani uchi wa mnyama na mambo mengine mengi mengi ya kimapenzi. Kidogo nichanganyikiwe.

Mama nisingeweza kumuuliza nikamuuliza mchumba wangu akaniambia nikweli aliwahi kuwa na mahusiano na Mama yangu hata kabla ya kukutana na mimi lakini alikua hajui kuwa ni Mama yangu mzazi, hata baada ya sisi kuwa pamoja alikua na Mama kama mchepuko wake. Kaniomba msamaha na kuniambia hakuna kitu tena kati yao, nimechanganyikiwa kwani nina mimba yake ya miezi sita na harusi ni mwezi wa tisa.

Niko njia panda sijui nifanye nini nimechanganyikiwa, nataka kuachana na mchumba wangu lakini nitasemaje, vipi huyu mtoto tumboni. Mchumba wangu ananiambia kua ananipenda na hawezi kuniacha, anatishia mpaka kujiua kama nikimuacha, hapa nawaza kila kikimuona Mama natamani hata kumpiga, nikiwaza kuhusu Baba kujua ana presha inaweza kumuua, naombeni msaada wenu nifanye nini maana nimechanganyikiwa.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA