NIFANYE NINI NIMEMFUMANIA MUME WANGU NA MCHUMBA WA SHOGA YANGU




Habari Kaka Iddi naomba nipostie katika ukurasa wako ili nipate maoni ya watu kaani nimechanganyikiwa na hali yangu na hali ya mume wangu. Mimi nimeolewa miaka kumi sasa naishi na mume wangu ndoa yangu inaenda vizuri sasa. Kama miaka miwili iliyopita nilisikia kuwa mume wangu ana tabia ya kutembea na mashoga kwa maana ya wanaume wengine, nilichunguza na kugundua kua ni kweli, kusema kweli nilichanganyikiwa lakini nilipata ujasiri wa kuongea naye.

Baada ya kuongea naye alikiri kweli alikua na tabia hiyo lakini aliniahidi kaacha na kusema kweli katika kipindi hiki cha miaka miwili sijamfumani wala kumhisi, nilijua ameacha kweli. Lakini sababu hasa ya kuamua kukufuata nikuwa kama miezi mitano hivi iliyopita rafiki yangu mmoja ambaye tunasali kanisa moja alitutambulisha mpenzi wake ni kijana tu wa makamo na huyo rafiki yangu ni kama mdogo wangu kwani nimemzidi zaidi ya miaka kumi hivyo ananiheshimu kama Dada yake pia.

Sasa baada ya kututambulisha kwakua wote tunasali Kanisa moja tukajikuta tunakua marafiki na kama unavyojua mkitoka wanaume wanakua marafiki pia, ingawa walikua hawajuani kabla lakini walijenga urafiki wa karibu, wakitoka pamoja na kufanya mambo kwa pamoja. Kwakua mume wangu ana magari mengi wakati wa maandalizi ya harusi alimuachia hata Gari moja huyo shemeji yangu mtatrajiwa.

Mwanzoni niliona kitu cha kawaida, sikushtuka kwanza kwakua nilishasahau tabia za mume wangu na pili kwakua najua huyo mchumba wake si shoga hivyo sikutilia shaka. Lakini juzi nilikua nafua nguo za mume wangu, wakati natoa Wallet nikataka kutoa hela ni mtume Dada sabuini kwani niliona haitatosha, wakati huo mume wangu alikuakalala kwani alirudi usiku kalewa nishamzoea kwa hilo.

Wakati natoa nikakuta laini imefichwa kenye vimfuko vya wallet ya mume wangu. Nilishangaa kwani mume wangu ana laini tatu tu za simu, sasa niliona ya nne, nikaamua kuichukua na kuweka kwenye simu yangu. Nilichokiona huwezi kuamini, yule shemeji yangu (Kamsave kwa jina leka kabisa) alikua anachat na mume wangu, anamuuliza kama jana kafika salama, anamuambia namna alivyofurahia na kumuambia kuwa anashida kidogo (kama mwanamke anavyoomba hela anavyomsifia mwanaume kwanza)

Kwamba kuna mambo yamepungua katika maandalizi ya harusi na alihitaji kama laki mbili, kuna mambo mengi ya kipuuzi ambayo aliandika na chat nyingine za nyuma niliona meseji ambazo huwezi andika hapa. Mimi si mvungaji nilienda na kumuamsha mume wangu na kumuuliza, alibaki anatetemeka tu mdomo na baadaye alikiri ni kweli kuwa anatembea na mchumba wa rafiki yangu. Alinisihi nisimuambie kwani yule sio shoga yeye ndiyo alimtamani na kuamua kumgeuza.

Aliahidi kua ataacha na anaamini kua hata huyo ataacha kama yeye akimuacha kwani hajaharibikiwa bado. Nilimuuliza wana muda gani akaniambia ni kama miezi minne sasa. Hapa nimechanganyikiwa nawaza je nimuambie Shoga yangu kuhusu mume wake mtarajiwa? Je kama akiacha atakuja kua kawaida, sijui nifanyeje kwakeli niwaache tu au la? Naomba ushauri wenu msinishauri kuhusu mume wangu kwani najua chakufanya tayari naomba ushuri kuhusu binti huyu ambaye ndiyo anaolewa mwezi ujao?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA