Soma hapa Kabla hujavunja ndoa yako WANAUME hatusamehei kitu hiki!


Kama umekutana na X wako kwa bahati mbaya, ukasalimiana naye, kwanza huna haja ya kupeana naye namba za simu, huna haja ya kuendelea kuwasiliana naye hasa kama umeoa au zaidi kama umeolewa. Lakini hata kama ukimpa namba za simu au alikua nazo hakuna haja ya kuwasiliana naye, hakuna haja ya kutumiana meseji. Hakuha haja ya kujibu SMS zake, hakuna haja ya kupigiana simu wala kuchat kwa namna yoyote ile!
Ila kama ikatokea akakutumia meseji acha kusema “Hakuna shida ni rafiki tu!” Ukaziacha katika simu yako kwakua tu hujafanya kitu kibaya, kwakua tu wewe unaona kuwa ni kawaida labda huna mpango wa kumrudia, unataiwa kujua kuwa hata kama wewe utaona kuwa ni kawaida lakini mpenzi wako/mume/mke wako hawezi kuona hivyo. Mawasiliano yoyote na X wako yataonekana kama ni usaliti na utakua ni ujinga kuyaendeleza wakati hamna kitu cha maana kati yenu.
Labda kama mna mtoto pamoja hapo hakuna namna au anakupa dili la kukutoa katika umasikini kabisa ili ukitoka hapo uwe Bakhresa, lakini labda kama ni Bosi wako mnafanya kazi pamoja na mnawasiliana mambo ya kikazi na si yeye kujishebedua umeamkaje, zatangu jana Happybirthday na vitu kama hivyo. Acha kabisa kwanini uharibu mahusiano yako kwa mtu ambaye mlishaachana.
Wewe unaona kama si ishu na najua kuwa hufanyi kitu kibaya, au unasema mliachana vizuri hamkugombana lakini mwenza wako hawezi kukuelewa. Hata mimi nikikuona unachata chata na X wako nitakuuliza kwanini kasahau nini, nini umekimiss kwake sasa wewe jifanye uzungu kuwa “Hakuna kitu kibaya!” Eti utemuelezea mke au mume wako kuwa hakuna kitu kibaya. Nakuambiaje acha huo ujinga hata kama hufanyi kitu kibaya mwenza wako lazima atashtuka.
Nimalizie tu kwa kukuambia huna hata haja ya kumuambia nilikutana na X wangu mjini tukasalimia, ndugu yangu kwanza atajihisi unajihami mshafanya yenu, acha ujinga huo, narudia acha ujinga huo, kama ni biashara kuna watu wangapi wa kufanya nao biashara mpaka ufanye na huyo X wako. Kumbuka utaharibu ndoa yako kwa SMS moja tu ya inayosema “Za tangu juzi?” kutoka kwa X wako.
Mimi nikiona meseji kutoka kwa X wako inauliza “Za tangu juzi?” Nitawaza juzi mlikua mnafanya nini? Kwanini akuulize, anashida gani nawewe? Ni kitu gani kimemfanya asikusahau, kwanini umempa namba, unataka mawasiliano naye ya nini? Tangu lini mmeanza kuwasiliana nae? Je umeniambia ili tu nikigundua nisitue au?
Kuna maswali mengi ya kujiuliza hivyohayo maswali, ili kutekwepa hembu ukikutana na X wako, msalimie, usimpe namba na kaa kimya humana haja ya kutangaza kuwa ulikutana naye labda kama unataka kuvunja ndoa au mahusiano yako! Narudia kabla ya kumpa namba yako tena X wako hembu jiulize utapata faida gani kwa kumpa, ni nini kimepungua katika kipindi chote hicho hamkua mnawasiliana na unampa ili nini unataka msalimiane ili nini? Wewe endelea tu kuwasiliana na huyo X wako ukiachika ndiyo utajua kwanini alikua ni X!
May be an image of 1 person and sunglasses

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA