Namna nilivyoweza kukabiliana na X wa mume wangu sasa ananipigia kunibembeleza mimi!


Najua utakua unanikumbuka kwani nilikusumbua sana mwaka jana, mimi ni yule ambaye mume wangu alizaa na X wake ambaye alikua mke wa mtu akaachika. Kila siku alikua akinipigia simu, kunitukana na kuniambia kua yeye ndiyo anapendawa, mimi ni kama House girl tu nalinda nyumba yeye anafaidi na kamwe hawawezi kuachana. Nilinunua Kitabu chako nikakupigia huku nikilia, nakumbuka uliniuliza nataka nini.
Ukaniambia nina machagua mawili, kwanza kumuona mume wangu mshenzi na kumuacha niendelee na maisha yangu au nimsamehe lakini ni nyamaze. Uliniambia huo mchepuko unafanya kazi ya kunitia mimi kisirani na nikishakipata basi nampelekea mume wangu hivyo sisi kila siku kugombana. Uliniambia kua kama X wake akinipigia simu akanitukana yeye anakua katoa kisirani chake na kunipa mimi.
Kwakua mume wangu ndiyo kasababisha yote hayo basi namuambia na tunagombana, ukaniambia kila siku tunaishia kugombana na kumzungumzia huyo X na kwakua mume wangu bado yuko naye basi akienda kwake anakua na amani kwania kimuuliza X wake anasema yeye hana shida wewe ndiyo tatizo, wanaongea naye wanafurahi, kule kunakua na amani wakati kwangu kuna waka moto.
Ukaniambia kama nabaki basi huyo X akipiga simu nipokee lakini niiweke pembeni nsiikate lakini nisimsikilize kabisa na akituma meseji basi wala nisizifungue na akiona simjibu, namdharau basi yeye atakua na kisirani na atampelekea mume wangu. Akimpeleka mume akirudi akiuliza namuambia mbona sina shida, yule ni mzazi mwenzio tena mmetoka mbali mimi sina tatizo. Ilikua ngumu sana kufanya hivyo lakini sikua na namana, ndoa naitaka, niliacha kuwa kisirani na kuwa na amani, silalamiki wala kuongea.
Uliniambia kama nina chakuongea nikupigie wewe na si kulalamika, kweli Kaka kamaulijua baada ya kukaa kimya yeye ndiyo akawa kisirani, kila siku wanagombana na mume wangu kuhusu mimi lakini mume akirudi namuambia sina tatizo. Wamegombana mpaka mume wangu kamtelekeza kwani anamsumbua sana. Mimi hata sijali juzi kanitumia meseji na namba ngeni baada ya kuona zakwake sijibu kwani sisomagi eti ananiambia “Kua na huruma hata huyu ni mtoto kama wako muambie mume wako atoe hata pesa ya chakula!”
Nilijikuta nacheka mwenyewe Kaka lakini kama ulivyoniambia nisijibu basi sijajibu na hiyo namba nimeiweka kwenye list yangu meseji zake zikiingia hata sifungui. Aliniumiza sana huyu dada, mapicha ya uchi na mume wangu, meseji zao za mapenzi kujaribu kunirusha roho lakini baada ya kusoma Kitabu chako na kujua namna ya kujipa furaha mwenyewe roho hairudi. Ushauri wako ni mgumu sana Kaka ila nimeweza na nina furaha na amani ya roho.
NB; Kwa ushauri tusichoshane, soma kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” bei yake ni shilingi elfu kumi tu, unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 a Tigo Pesa No. 0657-552-222 na kitabu unatumiwa kwa Whatsapp/Facebook/Email
May be an image of one or more people, flower and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA