Msifie mwanamke wako kwa namna ambayo ni tofauti na anvyosifiwa na wengine

 Msifie kitu ambacho ni muhimu sana kwake, najua ni muhimu kumsifia kuhusu muonekano wake, kumsifia kuhusu mavazi na vitu vingine vya kawaida, lakini wewe ni mume/mpenzi wake, unajua zaidi kuhusu yeye kuliko wale wengine. Dereva Bajaji anaweza kumsifia kapendeza, Shoga yake anaweza kumsifia kasuka vizuri, Bosi wake anaweza kumsifia kwa kufanya kazi vizuri lakini wewe kama mwanaume wake ni lazima kuonesha kuwa kuna kitu cha ziada.

content diverse family together in kitchen

Msifie namna anavyojituma kulea watoto, msifie kwa namna ambayo atajiona kabisa kuwa yeye ni wa kipekee na ana umuhimu sana kwako. Mmekaa kitandani au kwenye kochi, mvute karibu, chukua simu yako, fungua sehemu ya picha, angalia picha za watoto wenu na kisha muangalie usoni na muambie “Sijui hata bila wewe maisha yangekuwaje humu ndani?” Nyamaza, muache asubirie kwa sekunde kumi najua atauliza kwanini.

Muambie angalia hawa watoto, wewe ni Mama bora, yaani unakaa hapa nyumbani kutwa nzima huchoki, mimi masaa mawili tu nishachoka. Muambie hivyo Kama ni Mama wa nyumbani na kama anafanya kazi muambie sijui hata unafanyaje, unafanya kazi, unachoka kazini lakini ukirudi bado unakuwa Mama bora kwa wanangu.

Kuwa Mama ni kazi ambayo anaipenda pengine kuliko kitu kingine chochote kile, msifie hicho na onesha kuwa wewe hata kama humuambii mara kwa mara basi ni kitu ambacho unakikubali kutoka kwake. Kama hamna watoto tafuta kitu kingine, msifie namna alivyo mke bora, namna ambavyo anakurahisishia wewe kufanya kazi kwa yeye kuwepo.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA