KILA MWANAUME ANA AINA MOJA YA MATAMANIO YAKE KWA MWANAMKE

Mwanaume Katika kutamani Mwanamke huwa na aina moja ambayo humfanya kuwa dhaifu

Yawezekana ikawa miguu, Mapaja, Macho, Rangi ama wajihi "UREFU au UFUPI" na hawezi kuwa na vyote ila kimoja



Muda mwingine hata tembea ya Mwanamke ndiyo ikawa chanzo cha udhaifu wake kwa Mwanamke, Ila iko shida kubwa kwa wanaume nayo ni:-

Na hapo ndipo anguko la wanaume huinuka, Kwa sababu katika UTASHI ule ule ila wanawake tofauti na ukifuatilia unabaini hakuna anayemzidi mwenzie ISIPOKUWA ni ule ugonjwa wa wanaume kumlala Mwanamke na kumzoea kisha kukosa TAMAA juu yake

Mwanaume anapoacha kumtamani Mwanamke aliye nae maana yake ile tamaa halisi ya Mwanaume inatazama Mwanamke Mwingine lakini kwa UTASHI ule ule wa kile ambacho humpa udhaifu Mwanaume



Yaani unakuta Mwanaume ana wanawake watano na wote ni aina moja ya MATAMANIO lakini wote hao haoni aliye zaidi ya mwingine hata anaendelea kupepesa macho huko nje kutafuta Mwanamke Mwingine wa aina ile ile kama hao watano

Ndipo utakubaliana nami kwamba :-


Ukiona Mwanaume ameacha uzinzi ujue wewe ndiye kiboko yake, lakini kama kutwa mnagombana kisa usaliti ujue BADO TAMAA YAKE HUJAWA CHANZO CHA KUIMALIZA.