IKIWA MAKOSA KWENYE MAHUSIANO AMA NDOA YATAACHWA YAJISAMEHE MENYEWE BASI UJUE GANZI YA MAPENZI ITAKULA FURAHA NA AMANI YENU


💯
Kwanza nianze kwa kufafanua maana ya GANZI KATIKA MAPENZI:-
👉 Mtu yeyote aliyeumizwa na Mwenza wake halafu akabakia katika Maumivu kwa Muda mrefu, Mara nyingi hujikuta akikosa HAMU YA MAPENZI ambayo hupelekea GANZI ya kutokuwa na HISIA na mwenza wake.
Kinacho tuunganisha kwenye MAHUSIANO AMA NDOA ni mapenzi, Na Mapenzi mazuri yanazaliwa na HISIA wakati huo huo hisia ni zao la UPENDO.
Mara nyingi migogoro Kwenye Mahusiano na ndoa husababisha GANZI ya kuhitajiana ki mwili 👙
Ndo maana kama Wana Mahusiano ama ndoa wasipojua kurejeshana katika hali ya kuhitajiana ni anguko la UAMINIFU wao, kwani hamu ya MAPENZI ikidumu kwa Muda mrefu bila tiba huzaa hasira na siku zote maamuzi yaliyo tawaliwa na HASIRA huleta majibu yasiyo sahihi🤔
Kwani katika hali ya ki bin adam Mwanamke au Mwanaume anapokuwa ameumizwa na Mwenza wake na Mwenza huyo kutojua namna ya kumuondoa Mwenza wake katika Maumivu hayo automatically Mwenza aliyeumizwa hawezi kuwa na HISIA kwani Maumivu yatakuwa Kwenye akili na wakati huo MAPENZI NI AKILI.
Ndo maana USALITI mkubwa huanzia Kwenye migogoro ambayo haitatuliwi, Na mtu akijaribu kutoka nje ni rahisi kuhisi Kuna penzi tamu kuliko ndani na kumbe ni AKILI 🧠 yake kumuaminisha katika hilo, Kwa sababu Kule ndani kumevunja IMANI YA PENZI💔
Michepuko siku zote huleta FARAJA kwa wahanga wa MAPENZI kwani wanajua vita yenu ni neema kwao.
Huwezi kupewa penzi bovu kwa MCHEPUKO kwani akili yako haina ugomvi nae, lakini pia yeye yupo kwako kwa maslahi yake lazima atahakikisha unakuwa na AMANI japo tatizo lako lipo pale pale 😂
Maana kilichokutoa ndani mpaka kuangukia Kwenye usaliti ni migogoro ya Mahusiano ama ndoa yako, hujaimaliza bado ila unajaribu kupata RELIEF na ili uponye Mahusiano au ndoa yako basi unawajibika kutafuta suruhu ili kuirejesha FURAHA NA AMANI yenu💯
May be an image of 2 people, people sitting and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA